January 25, 2021

MKURUGENZI WA UINJILIST NA ELIMU AWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA

MKURUGENZI wa Uinjilisti na Elimu Kanda ya Kati, Mchungaji Nason Msanjila amewataka watanzania wanaofanya biashara kufanya biashara zao katika maeneo sahihi pamoja na kulipa kodi.

Mkurugenzi  Msanjila baye pia ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Uzunguni Jijini Dodoma,amesema watanzania wanatakiwa kufanya shughuri zao katika maeneo shahihi pamoja na kufuata taratibu zote zinazotakiwa wakati wa ufanyaji wa biashara sambamba na kulipa kodi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili alipokuwa kanisani hapo wakati wa ibada na kufindisha somo juu ya milango 12 ya mafanikio na baraka zake.

Kiongozi huyo amesema watanzania na watu wote kwa ujumla wanashindwa kufanikiwa kutokana na kutofanya shughuli zao katika maeneo rasmi na sahihi.

Amesema kuwa ili kuweza kufanikiwa katika kimwili ni lazima kufanya shughuli zako katika maeneo shahihi na rasm na hata Kiroho ni lazima kusikiliza sauti ya Mungu ilk iweze kukuongoza.

"Ili uweze kufanikiwa katika maisha nilazima ufanye shughuri harali na katika eneo rasm,pamoja na kutimiza vigezo ambavyo vinatakiwa ikiwa ni pamoja na kulipa kodi inayotamiwa.

"Ninaposema kufanikiwa hata katika mambo ya Kiroho ni lazima utembee katika maandiko na siyo kufanya kazi ya Mungu kisanii kwa lengo la kijipatia fedha au ujanja ujanja bali unatakiwa kutii na kuwa mnyenyekevu mbele ya Mungu"amesema Mkurugenzi Msanjila.

Akizungumzia kuhusu wiki ya Sheria iyozinduliwa leo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Jijiji Dodoma na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hasani,amesema bado kuna jukumu kubwa la kutoa elimu vijikini ili waweze kujua haki zao.

Amesema kuwa ili kuwa na nchi ya amani na utulivi lazina kuwepo na misingi imara ya itawala bora unaofuatia utekelezaji wa sheria na kanuni zake.

"Watu wengi hususani waishio vijijini bado hawajui sheria na ikiwa watapatiwa elimu juu ya mipaka na utendaji wa Jeshi la polisi, utendaji wa mahakama na utendaji wa watumishi wa serikali na wanasiasa hakika hakuna mtu ambaye anaweza kuonewa"amesema Kiongozi huyo wa Kiroho.

No comments:

Post a Comment

Pages