Mkurugenzi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG), Charles Meshack alielezea umuhimu wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ) mbele ya wadau wa misitu jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya TFCG na MCDI, John Salehe akichangia katika kikao cha siku moja cha wadau wa misitu kilichofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro Lucas Lemomo akielezea namna USMJ ilivyonufaisha wanavijiji wa halmashauri hiyo.
Washiriki wakiwa majadiliano ya sekta ya misitu, uhifadhi na mazingira wakiwa katika picha ya pamoja nje ya hoteli ya Morena jijini Dodoma.
NA SULEIMAN MSUYA, DODOMA
IWAPO
dhana ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ), haitasambazwa
kwenye vijiji vyenye misitu upo uwezekano wa hekta milioni 17 za misitu
kupotea ifikapo 2070.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhifadhi Misitu Tanzania
(TFCG), Charles Meshack wakati akizungumza na wadau mbalimbali kutoka
Serikali na sekta binafsi wanaohusika na sekta ya misitu waliokutana
jijini Dodoma.
Meshack
amesema Tanzania ina hekta za misitu milioni 48.1 ambapo hekta milioni
22 ni misitu ya vijiji hivyo USMJ ndio njia pekee inaweza kuinusuru
isiishe.
Amesema hadi
sasa USMJ ipo kwenye hekta milioni 5 pekee kati ya hekta milioni 22
iliyopo kwenye vijiji hali ambayo ni hatari katika rasilimali hiyo.
Meshack
amesema hofu ya kumalizika kwa misitu inaongezeka zaidi baada ya kuja
kwa GN 417 ambayo inaonekana kufanya kazi kwenye misitu iliyopo kwenye
USMJ pekee jambo ambalo limeanza kukatisha tamaa wanavijiji.
Amesema
takwimu zinaonesha kwa mwaka zaidi ya hekta 469,000 za misitu zinapotea
nchini hivyo Serikali inapaswa kuangalia upya GN 417 ili iweze kukidhi
haja ya kuendeleza rasilimali misitu.
"Ujio
wa GN 417 umezidisha hofu na kukatisha tamaa wanavijiji ambao wapo
kwenye USMJ kwani kwa sasa mazao ya misitu hayatoki kwani misitu isiyo
na USMJ takribani hekta milioni 17 uvunaji wake hauna mazingira magumu,"
amesema.
Amesema
kumekuwepo na kasi kubwa ya uvunaji mazao ya misitu kama mkaa na mbao
kwenye maeneo ambayo hayana USMJ na msukumo mkubwa ni kutotumika GN 417
kwenye maeneo hayo.
"Hali
inaonesha kuwa kama hakutakuwa na USMJ miaka 50 ijayo misitu itakuwa
imeisha na sababu kubwa ni kilimo na ufugaji ambavyo kwa upande fulani
vinaonekana kuchochea maendeleo," amesema.
Mkurugenzi huyo amesema zipo changamoto za kiutendaji na kisera ambazo msingi mkubwa ni kuongeza uzalishilaji kwa sekta husika.
"Hizi
changamoto zinaweza kupata muafaka kwa wadau kujadiliana na kuwa na
kauli moja ambayo kila sekta itazingatia eneo lake na sio kushindana.
Lakini
pia changamoto ya GN 417 inapaswa kuangaliwa kwa jicho la huruma ili
kutokatisha tamaa vijiji vinavyotekeleza USMJ," amesema.
Meshack
amesema changamoto nyingine ni misitu ya asili kutopewa kipaumbele kama
isiyo ya asili jambo ambalo linaondoa ari ya uhifadhi.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Morogoro, Lucas Lemomo amesema USMJ umechangia
mafanikio mengi katika vijiji vitano vilivyopo kwenye halmashauri yake
hivyo ni jambo la kuungwa mkono.
Lemomo
ambaye ni Diwani wa Kata ya Matuli amesema kumekuwepo na changamoto
kutoka Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS) kushindwa kutoa vibali
vya kusafirisha mazao ya misitu kwa haraka.
"Lakini
katika hali ya kushangaza TFS haohao wanatoa vibali kwa haraka kwa
wafanyabiashara wanaonunua nje ya maeneo yenye USMJ hali ambayo
inakatisha tamaa," amesema.
Diwani
wa Kata ya Kisanga Halmashauri ya Kilosa mkoani Morogoro, Hassan
Kambenga amesema wilaya hiyo ina vijiji 20 vinavyotekeleza USMJ na
asilimia kubwa wananchi wamenufaika kwa huduma nyingi.
Amesema
Serikali inapaswa kutenga bajeti kuhakikisha kuwa USMJ inasambaa kila
kona ya nchi kwa kuwa ina faida na kuachana na kuja na sheria zenye
kukwamisha mafanikio hayo.
"Hili
la wavunaji wa mazao ya misitu waliopo kwenye USMJ kutohudumiwa na TFS
vizuri lipo hadi Kilosa hivyo tunaomba wabadilike kwani wanatoa tafsiri
mbaya," amesema.
Naye
mnufaika wa USMJ, Kulangwa Ganda kutoka Kijiji cha Kitunduweta Wilayani
Kilosa amesema wamenufaika hivyo kuitaka serikali iendeleze dhana hiyo.
"Niombe Serikali isiwe sehemu ya kikwazo kwenye miradi hii ya USMJ kwani ina matokeo chanya yanayopaswa kuendelezwa," amesema.
No comments:
Post a Comment