April 22, 2021

MILIONI 134 ZAOKOLEWA NA TAKUKURU MKOA WA PWANI

 


Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani Suzana Raymond akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake hawapo pichani juu ya utekelezaji ya mapambano ya rushwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi machi mwaka 2021. (Picha na Victor Masangu).

 

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI

 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani katika kushugulikia malalamiko yaliyowasilishwa imeweza kufanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya shilingi  milioni 134 ambazo zilikuwa zichepushwe au kufanyiwa ubadhilifu na matapeli  kinyume kabisa na sheria za rushwa namba 11 ya mwaka 2007 .

 

 

Akizungumza na wandishi wa Habari Ofisini kwake Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Raymond wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji kwa robo ya mwaka huu wa 2021  kwa kipindi cha kuanzia Januari mpaka machi ambapo amedai kuwa fedha hizo zote wameweza kuziokoa kutokana na kazi ambayo imefanywa na ofisi yake kuanzia ngazi za Wilaya hadi Mkoa.

 

Mkuu huyo alibainisha kwamba katika juhudi hizo ambazo zilifanywa na Ofisi ya Takukuru Wilaya ya Bagamoyo alisema wao walifanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi zaidi ya shilling milioni 57 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya fedha za michango ya mafao ya NSSF na PSSSF kwa watumishi wa shule ya sekondari ya Eangle ya Wilayani humo.

 

“Kwa kweli kiasi hiki cha fedha cha zaidi ya milioni hamsini na saba kiliweza kuchepushwa na kwamba kilikuwa bado hakijawakilishwa na mwajiri ambaye ni mmmiliki wa shule hiyo ya sekondari kwenye mifuko husika hivyo Ofisi yangu katika kulifuatilia suala hili tuliweza kubaini kuwepo kwa hali hiyo,”alifafanua Mkuu huyo.

 

Pia mkuu huyo alifafanua kwamba waliweza kufanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 14 ambazo zilitakiwa kutumika katika uchimbaji wa visima vinne katika Wilaya ya Bagamoyo ambapo zilitolewa kwa baraza kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA)  kutoka kwa mfadhili ambaye ni raia wa Oman kwa ajili ya wananchi wa kata ya Zinga.

 

Aidha Mkuu huyo alisema Ofisi ya Mkuranga waliweza kuokoa kiasi cha shilingi milioni ishirini na moja ambazo wakulima waliweza kudhulumiwa na baadhi ya viongozi wa bodi za AMCOS za maeneo ya Njopeka Chungulo, njia nne pamoja na Tunduni Magawa.huku katika Ofisi ya Kibiti yenyewe ikifanikiwa kuokoa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni sita.

 

Kwa uapnde wa Wilaya ya Kisarawe Takukuru iliweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kufanikiwa kuokoa jumla ya kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni kumi  zikiwa ni fedha ambazo zilitolewa na serikali na fedha za wananchi zilizotumika na kufanyiwa ubadhilifu na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

 

Pia katika  hatua nyingine Mkuu huyo alibainisha kuwa Ofisi ya Wilaya ya Rufiji iliweza kurejesha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mbili ambazo zilikuwa zimekopeshwa kwa ajili ya vikundi wanawake, vijana pamoja ana kundi la walemavu, ambazo fedha hizo zimerudishwa baada ya kufanya ufuatiliaji wa kina na kubaini hali hiyo.

 

 

Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Pwani imetembelea miradi ya maendeleo 15  katika sekta ya maji, ujenzi, elimu ambayo imegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili na kubaini kuwepo kwa mapungufu na kasoro mbali mbali ambazo zimepelekea kwa baadhi ya miradi kutokuwa na tija na kushindwa kukamilika kwa wakati.

 

No comments:

Post a Comment

Pages