April 27, 2021

Taasisi ya Kielimu ya Kaizirege na Kemebos yajivunia mafanikio yake


 Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya
Kaizirege na Kemeboshi, Eusto Ntagalinda (katika). Kulia ni Shekhe wa Mkoa wa Kagera, Harouna Abdalla Kichwabuta ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya shule ya sekondari Kaizirege na shule ya Kemebos.


 

 Na  Lydia Lugakila, Bukoba


Taasisi ya Kielimu  Kaizirege na Kemebos iliyopo mkoani Kagera imeshuhudia kukua kwa mradi katika huduma  hiyo baada ya kuzalisha vijana wenye uwezo kitaaluma na kupata tuzo mbali mbali za ushindi kitaifa.


Akisoma lisala  katika mahafali ya tano ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Kaizirege na ya nne kwa  shule ya Kemebos Meneja wa shule hiyo  Eulogius William Katiti amesema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo 2007 chini ya mkurugenzi wake Eusto Kaizirege Ntagalinda wakati huo  kukiwa na shule ya Kaizirege tu  walianza na shule ya msingi ambapo hadi Sasa ni  miaka 14 wakiwa wamefanikiwa kuwa na kidato cha sita  na kuzaa shule ya Kemebos ambayo imeanzia awali Hadi kidato Cha sita.


Katiti amesema kuwa katika miaka hiyo 14 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo  wameendelea kuona ufaulu mzuri kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na ule wa mitihani ya ndani na ya taifa mara kadhaa kwa kushika kati ya nafasi za juu kwenye 10 Bora kitaifa pamoja na kutunukiwa tuzo mbali mbali kutokana na ubora wa taaluma shuleni hapo.


Aidha amempongeza mkurugenzi wa taasisi hiyo  Eusto Kaizirege Ntagalinda kwa kuhakikisha anakuwa na walimu mahili wenye nidhamu ya kazi na walio tayari kutimiza wajibu wao.


" eneo hili limeutambulisha mkoa wa Kagera kitaifa na kimataifa kwani taasisi hii imesaidia kutoa ajira rasmi, na ambazo siyo rasmi kwa vijana wengi na hivyo kupunguza idadi ya vijana wasio kuwa na ajira "alisema Katiti.


 ameongeza kuwa taasisi hiyo  imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi mbali mbali na hivyo  kukuza pato la taifa.


Aidha akitaja Mambo yaliyochochea mafanikio upande wa taaluma meneja huyo ameongeza kuwa ni pamoja na kuwa shule yenye miundo mbinu rafiki,  iliyokamilika pamoja na utaratibu wa wafanyakazi kulipwa malipo yao kwa wakati ambapo pia kumeshuhudiwa wanafunzi 5 waliohitimu katika shule ya Kaizirege na Kemebos kurejea kupata ajira shuleni hapo baada ya kuhitimu vyuo vikuu.


Kwa upande wake Mgeni rasmi katika mahafali hayo Shekhe wa mkoa wa Kagera Harouna Abdalla Kichwabuta amewahimiza wahitimu hao kuiheshimu misingi ya dini kwani mafanikio makubwa yanakuja kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu.


"Namshukuru mkurugenzi Eusto Kaizirege kwa uwekezaji huu hakika mkoa wa Kagera umeng'aa niwaombe wahitimu msivunje miiko endeleeni kuwa mwanga katika kuongeza ufaulu" alisema Shekhe Kichwabuta.


Shekhe huyo amewataka wazazi na walezi kuweka mkakati wa uchangiaji pesa kwa watoto wao wanaotaraji kwenda shule kuliko kuwekeza nguvu kubwa katika starehe ikiwemo harusi na kadhalika.


Hata hivyo jumla ya wahitimu 217 kutoka taasisi hiyo wamehitimu huku wakisubiri kufanya mitihani yao baada ya maandalizi kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Pages