May 04, 2021

Prof. Mkumbo: nimefurahishwa na utendaji wa TBS

 


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo. (Picha na Eliud Rwechungura).

 

 

NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limepongezwa kwa kasi ya utendaji kazi wa kuhakikisha bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi na zile zinazozalishwa nchini zinakuwa na ubora unaokubalika.

Haya yamesemwa jijini Dar es Salaam jana, na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea Shirika hilo, halina rekodi ya bidhaa ambayo hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Prof. Mkumbo alisema kwa hali hiyo inamaanisha kwamba kuna wafanyakazi wanadhibiti uingizwaji wa bidhaaa za kutoka nje ya nchi na zinazozaliehwa hapa nchini.

Alisema shirika hilo linatekeleza mambo yake vizuri na kuahaidi kulipatia  ushirikiano kuona kwamba  linanafasi nyingine za kushiriki kikamilifu katika kuwezesha biashara ndani ya Sheria zilizopo katika ubora unaotakiwa na serikali.

"Nawapongeza TBS kwa kazi Nzuri waliyofanya za  kuhakikisha bidhaa zinazoingia kutoka nje na ambazo zinazalishwa  hapa zinazingatia Ubora  hivyo mafanikio yao ni makubwa hapa nchini,"alisema.

Aliongeza kuwa baada ya kukutana na wafanyabiashara leo (jana), pale Bandarini TBS ilitajwa kwa uchace  katika malalamiko yao na kwamba hatua hiyo ilintia moyo kwa kuona wanafanyakazi nzuri.

Alisema wamekubaliana na TBS kuongeza Bodi katika kuhakikisha mnafanya kazi kwa spidi kubwa ili wafanyabiashara wanaofanya biashara waweze kulewa huduma mapema iwezekanavyo.

"Nimewasisitiza watu wa TBS umuhimu wa huduma bora kwa wateja kwa kuwa wanafanya kazi na wafanyabiashara ni muhimu kuboresha huduma kwa wateja hilo ni jambo la Msingi,"alisema.

Aidha aliaidi kuyafanyia kazi kwa haraka iwezekanavyo mambo mawili yanayohusu Shirika hilo ikiwemo suala la uundwaji wa  bodi ya wakurugenzi na kuhakikisha wanafanya marekebisho ya Sheria mapema ambayo unahitajika kuboresha utendaji kazi.

No comments:

Post a Comment

Pages