May 07, 2021

UFUNGUZI WA MAONESHO YA MAKISATU DODOMA

 

HAMIDA RAMADHANI, DODOMA


WAZIRI wa Elimu Sayansi na Techinologia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetenga Jumla ya Shilingi Bilioni 3.2 kwaajili ya kuwaendeleza wabunifu walioshinda mashindano ya kitaifa ya kisayansi na Teknolojia (MAKISATU) 2019 mpaka 2020.


Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati akifungua Maonesho ya Mashindano ya Kisayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliofanyika kitaifa Jijini Dodoma.


Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kutenga fedha kwaajili ya kuendeleza Ubunifu nchini kupitia vituo vya kuendeleza Teknolojia na Ubunifu.


"Niwaombe wabunifu wote nchini kujitokeza ili Ubunifu wao uweze kuonekana na uweze kutambulika msijifiche jitokezeni tuone Ubunifu kwani mkitambulika mtaendelezwa,"amesema Profesa Ndalichako.


Hata hivyo amezitaka Taasisi zinazohusika na masuala ya Teknolojia na Ubunifu nchini kuongeza kasi ya kuwatambua na kuwaendeleza wabunifu wote nchini na kuhakikisha kwamba Ubunifu wao unalindwa ipasavyo.


Amesema kwamba anatambua  kunamuongozo wakutambua wabunifu katika Halmashauri  hivyo wasimamie kuona muongozo huo unafanya kazi.


"Ninaimani kwamba tunawabunifu wengi hapa Nchini kwetu Tanzania kuliko wale ambao tumeweza kuwainua au kuwaibua katika Mashindano kama haya ya kitaifa,"amesema .


Na kuongeza kuwa " Mashindano ya kitaifa ni njia mojawapo lakini mfumo ambao tumeshautengenezea muongozo na upo katika Halmashauri tuakikishe tunausimia vizuri ili wabunifu wote waweze kutambuliwa na kuendelezwa," amesema.


Pia ameiagiza Tume ya Sayansi na Teknolojia kuhakikishe vikwazo vyote vinavyowekwa katika usajili wa bunifu za watanzania vinaondolewa ili kuwezesha Bunifu hizo zinaleta faida kwa nchi na zinafahamika kimataifa.

Amesema kuwa Serikali Pamoja na wadau kwa Pamoja wanatumia Fedha nyingi ili kuendeleza Bunifu zinazobuniwa na watanzania na Lengo lake ni kuhakikisha zinafika Mbali na kuisaidia jamii na wabunifu kwa Ujumla.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Dkt Leonard Akwilapo amesema Tangu kuazishwa kwa Mashinda no hayo ya Ubunifu, Bunifu 130 zilizoshinda zinaendelezwa na Serikali huku Bunifu 26 zikiwa zimefikia hatua ya kubiasharishwa.


Naye Mussa Dotto ni Miongoni mwa wabunifu waliopo katika Mashindano hayo ambaye ni Muhitimu kutoka chuo cha Mzumbe aliwahi kushiriki maonyesho hayo na baadae kuboresha bunifu yake ambapo amesema yupo hapo kwaajili ya kuonyesha bunifu yake na atakapo shinda atengeneze nyingine zaidi.

" Mimi niko hapa kwenye Maonesho hii ni mara yangu ya pili na nimekuja kuonyesha bunifu yangu ya gari shamba na ninaimani nitashinda na kushinda kwangu itakuwa ni mkombozi kea Mkulima wa Jembe la mkono,"amesema Mussa.

No comments:

Post a Comment

Pages