May 27, 2021

Vyuo Vikuu vyahimizwa kufanya tafiti zenye tija kijamii na kiuchumi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mhadhiri Mwandamizi Idara ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Lilian Kaale alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kufunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na chuo hicho.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (katikati), akipata maelezo alipotembelea banda la NMB kabla ya kufunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, akifunga Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (kulia), akimkabidhi tuzo ya
ya Mtafiti Bora aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na chuo hicho.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (kulia), akimkabidhi tuzo ya Mtafiti Bora wa Mwaka Dk. Samwel Mchele Limbu, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

 

Mshindi wa Kwanza wa Mradi Bora wa Utafiti Dk. Mwita Mangora, akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 20 kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


Hussein Ndubikile, Dar es Salaam 


Vyuo Vikuu nchini vimehimizwa kujikita katika tafiti na bunifu endelevu zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali za jamii pamoja na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Joyce Ndalichako wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema kuwa vyuo hivyo vinatakiwa kufanya tafiti zitakazoweza kujitofautisha na taasisi zingine za elimu na kwamba zilenge katika kuisaidia jamii kupunguza changamoto na kuleta maendeleo.

" Vyuo Vikuu lazima vifanye tafiti za kuilenga jamii visipofanya vitakuwa havina utofauti na shule za kawaida tafiti ziibue majibu kusaidia nchi kimaendeleo," amesema Dkt. Akwilapo.

Amebainisha kuwa tafiti zinazofanywa na vyuo vikuu huvisaidia kujiweka karibu na jamii pamoja na kujitangaza kimataifa kwani matokeo ya tafiti husambazwa sehemu mbalimbali.

Amekipongeza chuo hicho kwa kuandaa maadhimisho hayo kwa kutenga fedha zake za ndani huku kwani kinaonyesha dhahiri kilivyojipanga kutatua kero za jamii na kuchochea maendeleo ya viwanda.

Ameongeza kuwa wizara hiyo iko pamoja na UDSM kimahusiano na kwamba ni mojawapo ya chuo kinachotambulika kwa ufanyaji tafiti zenye tija kwa nchi.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye amesema maadhimisho ya kilele cha wiki hiyo yamelenga kuonyesha jinsi gani UDSM haijajitenga na jamii kupitia tafiti na bunifu zilizowasilishwa.

Amesisitiza kuwa wiki hiyo ni kiungo muhimu kati ya chuo na umma huku akiwapongeza washindi na walioshinndwa kuendelea kutafuta kuendelea kutafuta mawazo mengine ya utafiti na ubunifu.

Amefafanua kuwa chuo hicho kitatekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Maajaliwa linaloelekeza kuhakikisha tafiti wanazofanya zinakuwa na mwelekeo wa kiuchumi.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa Utafiti wa chuo hicho Profesa Bernadeta Killian amesema maadhimisho hayo yalianza mwaka 2015 yakijulikana kama wiki ya utafiti na baadaye yalifanyiwa maboresho ya jina lake.

Profesa Bernadeta amesema jumla ya kazi 218 za vitengo ziliwasilishwa zikiwemo za wafanyakazi na wanafunzi ambapo washiriki 1,000 wamehudhuria wiki hiyo.

Aidha, amesema maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo Utafiti na Ubunifu kwa Maendeleo ya Viwanda na Jamii Tanzania na kwamba kulikuwa na mawasilisho ya makampuni, wanafunzi na viongozi wa serikali
 
Katika kilele hicho tuzo na hundi za fedha taslimu zilizotolewa ikiwemo ya Jarida bora la mwaka 2021, Tuzo ya Idara iliyoleta fedha nyingi za utafiti chuoni hapo ilikwenda kwa Shule ya Biashara iliyoleta Sh Bil 2.5, Mtafiti hodari wa mwaka 2021 imechuliwa na Dkt.Samwel Lyimo amepata Sh mil 5.

Tuzo nyingine ni ya Mbunifu hodari aliyepata ni Dkt.Budeba kutoka Chuo cha Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE) amepata tuzo ya ngao na hundi ya Sh mil 5 huku Tuzo ya Miradi Bora ya Makundi ikienda kwa  Mshindi wa kwanza Dkt.. Mwita Mangira aliyepata hundi ya Sh mil 20.

No comments:

Post a Comment

Pages