May 07, 2021

WALIOWABEBESHA MIMBA WANAFUNZI KUSAKWA

 


Mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji na diwani wa kata ya Rulanda Evart Ernest Tilwetwa.

 

Na Lydia Lugakila, Muleba

Madiwani katika Halmashauri  ya Muleba mkoani Kagera wameendelea na taarifa rasmi za kuwatafuta wahusika waliowabebesha mimba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo huku watu  16 wakiwa wanasakwa na mmoja kukamatwa kwa matukio hayo.

Ikiwa jumla ya kesi 32 zimeripotiwa na mtu mmoja kutoroka, tayari kesi 3 ziko mahakamani na kesi moja imehukumiwa ambapo shule wanazotoka wanafunzi hao waliobebeshwa mimba  ni jumla ya  shule 23 zikiwemo msingi na sekondari.

Akieleza taarifa hiyo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya muleba Evart Ernest Tilwetwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji  pia diwani wa kata ya Rulanda amesema kuwa kutokana na uwepo wa wimbi la wanafunzi kubeba mimba kwa shule za msingi na sekondari katika baadhi ya  wilaya mbalimbali mkoani Kagera wilaya  hiyo iliunda kamati maalum ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inafuatilia kuzuia na kudhibiti mimba shuleni, ikiwa ni pamoja na watu wanaohusika  kubebesha   mimba wanafunzi walifuatiliwa na kukamatwa na baadhi yao kupelekwa katika vyombo kisheria.

Amesema kuwa kamati hiyo ilifanikiwa kukamatwa kwa mtu mmoja na mmoja kutoroka huku 16 wakiendelea kusakwa.

Evert ameongeza kuwa, kufuatia mikakati kabambe waliyonayo madiwani hao kwa kushirikiana na wadau pamoja  wananchi wameendelea kuhamasisha na kuonyesha madhara ya mimba  idadi ya wanaobeba mimba mwaka baada ya mwaka imeendelea kupungua toka mwaka 2019 hadi Aprili 2021.

" shule za msingi kwa mwaka 2019 walibeba mimba wanafunzi 7, sekondari wanafunzi 22 jumla 29 ambapo mwaka 2020 shule za msingi walipungua hadi kufikia 5  sekondari 18 jumla yake 23 na hadi mwaka 2021 mwenzi aprili shule za msingi hakuwepo mwanafunzi hata mmoja aliyebeba mimba huku sekondari wakiwa 5" alisema diwani huyo.

Aidha amesema kuwa jitihada hizo zimeleta ufanisi mkubwa katika wilaya hiyo  licha ya ugumu huku akitaja changamoto kubwa inayosababisha kufifisha jitihada hizo  kuwa ni pamoja na wazazi wa mabinti kwani pale inapotokea mtoto kabeba mimba na wakaonekana ofisini viongozi uchukua hatua za kuwapeleka katika vyombo vya sheria,  ambapo baadae wahusika waliombebeshwa mimba mwanafunzi upita mlango wa nyuma na kukutana na wazazi wa familia ya mwanafunzi ili wakatoe chochote na kesi ipuuzwe au wakati mwingine binti anakuwa hajulikani halipo na yule aliyembebesha mimba hapatikani jambo linalosababisha ushirikiano kukosa.

Hata hivyo diwani Ernest amesema madiwani hao wataendelea kutoa elimu katika jamii ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kuwabaini na kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wote wanaohusika na matukio hayo na kuongeza kuwa tayari wamebaini kundi la  waendesha pikipiki maarufu BODA BODA na vijana wa kawaida wenye uwezo na wamiliki wa vioski wanafanya ushawishi kubwa kwa watoto hao.

No comments:

Post a Comment

Pages