May 19, 2021

WANAFUNZI ARUSHA WAPATIWA ELIMU YA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA VIUMBE

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai Iliyopo jijini  Arusha Dkt. Christine Ngereza (kulia) akizungumza na wanafunzi waliotembelea makumbusho hiyo katika  kilele cha maadhimisho ya siku hiyo  yaliyoadhimishwa duniani kote leo. 
Wanafunzi wakiwa mbele ya Makumbusho ya Viumbe Hai iliyopo jijini  Arusha baada ya kuitembelea katika kilele cha  Maadhimisho.ya  Siku ya Makumbusho yaliyoadhimishwa duniani kote leo.



Na Dotto Mwaibale  


WANAFUNZI jijini Arusha wamejengewa uwezo wa kujua Makumbusho ya Taifa katika kilele cha maadhimisho  yaliyoadhimishwa duniani kote leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo jijini Mkurugenzi wa Makumbusho ya Viumbe Hai iliyopo jijini  Arusha Dkt. Christine Ngereza alisema moja ya shughuli walioifanya  ni kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule mbalimbali waliofika katika maadhimisho hayo.

" Tumekuwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali ambao tumewapa elimu kuhusu masuala ya makumbusho ambayo wameyafurahia" alisema Ngereza.

Alisema kumekuwa na changamoto kwa wanannchi kutojua masuala ya makumbusho kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.

Alisema ni vizuri sasa kukawa na makongamano, semina na midahalo maeneo mbalimbali ya kufundishana masuala ya makumbusho ambayo ni muhimu kwa nchi yoyote duniani.

"Katika maadhimisho haya kitu kikubwa kilicho nifurahisha ni jinsi wanafunzi walivyo kuwa na kiu ya kuuliza maswali mengi kutaka kujua makumbusho" alisema Ngereza.

Ngereza alisema  mwaka huu Tanzania imeungana na nchi zaidi ya 158 duniani kuadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu isemayo The Future of Museums Recover and Re imagine.

Akizungumzia kuhusu  Makumbusho hayo alisema kazi kubwa walioifanya ni kutoa elimu ya kuwajengea uelewa wananchi juu ya kutembelea makumbusho  kama sehemu ya kupata elimu na burudani kuhusu urithi wa nchi wa kale na wa Sasa wa Asili Mazingira Utamaduni Sayansi,Teknolojia na Historia.

Dkt. Tungereza alisema tangu asubuhi makumbusho ya jijini Arusha ilikuwa wazi ambapo wananchi wakiwepo wanafunzi walipata fursa ya kuitembelea. 

No comments:

Post a Comment

Pages