May 27, 2021

ZAWADI MISS KAGERA 2021 HII HAPA


 Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo akizunguza baada ya kuzindua zawadi ya gari kwa ajili ya mshindi wa taji la miss Kagera 2021.

Mkuu wa wilaya ya katika majaribio ya gari hilo jipya.
Mwekezaji na muandaaji kutoka Zachwa Investment Muganyizi Zachwa akizungumza katika uzinduzi huo.

 

Mratibu wa shindano hilo  Regina Samweli Zachwa akitoa ufafanuzi wa shindano hilo.

 

Zawadi ya gari kwa ajili ya mshindi wa kwanza wa shindano la miss Kagera 2021.

 

 

Lydia Lugakila, Bukoba

Zawadi ya gari mpya yenye thamani ya shilingi milioni 18 yatambulishwa rasmi kuelekea shindano la Miss Kagera itakayotwaliwa na mshindi wa kwanza wa shindano hilo.

Akitambulisha zawadi hiyo ya gari mpya aina ya Rectus yenye thamani ya shilingi milioni 18 mratibu wa shindano la miss Kagera 2021 Regina zachwa kutoka Zachwa Investment kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo Serengeti Breweries Ltd wametaja kukamilika kwa mchakato mzima wa shindano hilo.

Regina amewashukuru wabunge wa mkoa huo pamoja na serikali kuunga mkono suala hilo huku akieleza  maadalizi hayo kuiva na kuwa wanategemea ushindi mkubwa kwani mpango wao ni kuifia miss Tanzania 2021.

Amesema mwanzoni walianza na kamati ya miss Tanzania ambayo kwa kushirikiana na wizara ya michezo tamaduni na sanaa ambapo walikubakiana kurudisha heshima ya miss Kagera.

" Miss Kagera ya mwaka huu itakuwa ya tofauti Sana kwani tayari maandalizi yamekamilika    tunategemea mshindi atakayepatikana atauwakilisha mkoa wa Kagera" alisema Regina

Akizindua rasmi zawadi hiyo ya gari mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amewapongeza waandaaji wa shindano hilo na kuwa tayari serikali inathamini mashindano hayo kwani yanaiweka Tanzania katika ramani nzuri kwa kutambulika dunia nzima .

Kinawilo amesema serikali imeruhusu mashindano hayo kuendelea na kuomba mshindi atakayepatikana kuhakikisha anatangaza vivutio na rasilimali zikizopo mkoani Kagera huku akiwataka wazazi kulipa kipaumbele suala hilo na kuondoa fikra mbaya iliyojengeka katika jamii kuwa Umiss ni Uhuni.

Aidha kwa upande wake muandaaji na mwekezaji ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha redio cha Kasibante Muganyizi Zachwa amesema shindano hilo kwa mwaka huu litakuwa la tofauti na yaliyowahi kufanyika hivyo wasichana wajitokeze kwani licha ya zawadi ya gari Kuna zawadi nyingine kabambe.

Naye Meneja vipindi wa Kasibante FM Redio ambaye ni moja kati ya waandaaji amewaomba wazazi kutoweka vikwazo kwa mabinti zao walio tayari kujitokeza katika kinyanga'nyiro cha taji hilo kwani kwa kufanya hivyo ni kubinya ndoto za vipaji vyao.

Hata hivyo kamati hiyo ya shindano la Miss Kagera limeweka wazi ratiba ya shindano hilo kwa wilaya za mkoa huo ambapo Mei 28 na 29 mwaka huu shindano hilo litaanzia wilaya ya Biharamulo na Ngara na mwezi julai itakuwa Karagwe na Kyerwa huku kilele cha shindano hilo kikiwa ni Agosti 08, 2021 na kufanyika katika Manispaa ya Bukoba mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Pages