HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2021

ADHABU KALI KUWASHUKIA WATAKAOSABABISHA KELELE NA MITETEMO

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Saidi Jafo akitoa Taarifa kwa Umma ya Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira utokanao na Kelele na Mitetemo kwa waandishi wa habari leo Juni 29, 2021 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


OFISI ya Makamu wa Raisi,Muungano na Mazingira kwakushirikiana na Ofisi ya Rais Tamisemi,Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji,Wizara ya Afya,wizara ya Elimu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa maelekezo mbalimbali  katika kuhakikisha inalinda afya ya Jamii kutokana na athari zitokanazo na kelele na mitetemo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemo  na hivyo kusababisha athari za kiafya na kimazingira kwa jamii.

 

Aidha amebainisha kuwa  maeneo yanayoongoza kwa kulalamikiwa na kelele na mitetemo ni nyumba za starehe na burudani pamoja na nyumba za ibada huku akitoa wito kwa viongozi wa dini kutoa elimu namna ya kupunguza sauti katika nyumba za ibada.


Katika hatua nyingine amesema kuwa kwa yeyote atakayesababisha  kero  zitokanazo na kelele na mitetemo kinyume na kanuni za usimamizi wa mazingira za mwaka 2015 atakuwa amevunja sheria na adhabu yake ni faini ya sh. milioni moja au kifungo cha miezi sita pamoja na kutaka Mamlaka za Tamisemi kusimamia utekelezaji wa kanuni za usimamaizi wa mazingira za udhibiti wa kelele ya mwaka 2015..

 

Jafo ameeleza kuwa katika kipindi cha Januari hadi Machi 2021,NEMC wamepokea malalamiko 93 kutoka Kanda ya Kati (30), Kanda ya Kaskazin (12), Kanda  ya Ziwa (21), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (6) na Kanda ya Mashariki 31.


Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima alisema kuwa takwimu za shirika linalosimamia mazingira katika bara la ulaya zinaonesha kelele husababisha vifo vya mapema vya watu 16,600 na wengine 72,000 hulazwa hospitalini kila mwaka kutokana na madhara ya kelele.


"Kelele zilizopita  zilizopita kiwango stahiki Cha afya ni chanzo Cha magonjwa ya hatari kama iliyotajwa kwenye takwimu kutoka bara la ulaya" amesema DK Gwajima.

 


Hata hivyo wananchi wametakiwa kutoa taarifa  kuhusu kero ya mitetemo na kelel kwa ofisi za serikali za mitaa au baraza la uhifadhi wa mazingira nchini kwa kupiga simu bure kupitia namba 0800110115 aua 0800110117 au 08001106.

No comments:

Post a Comment

Pages