June 17, 2021

Manispaa ya Bukoba yaagiza shule kuwa na mabaraza ya Watoto

 

 

Katibu Tawala Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Kadole Kilugala akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.


Na Lydia Lugakila, Bukoba


Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Kadole Kilugala, ameagiza shule zote katika Manispaa ya Bukoba  ambazo hazina mabaraza ya watoto kutengenezeza mabaraza hayo mara moja ili kuwawezesha watoto kupata fursa ya kuongea mambo yanayowahusu na kutoa mapendekezo yao.

Kilugala ametoa maagizo hayo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru maarufu Mayunga ulipo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba.

Kilugala amesema kuwa shule zote katika Manispaa ya Bukoba ambazo hazina mabaraza ya watoto ngazi ya shule zinatakiwa kuunda mabaraza hayo ili kuwa kuwawezesha watoto kupata mabaraza ngazi ya kata, kupata viongozi na wajumbe ngazi ya Halmashauri na wilaya hadi ngazi ya taifa ili watoto hao waweze kusikilizwa matakwa yao haraka.

" watoto watapata fulsa ya kuongea Mambo yao yanayowahusu na kutoa mapendekezo yao na serikali kuweza kuwasimamia kwa sababu kwa Sasa sera ya serikali ni kuwawezesha watoto kutambua haki zao, kujua thamani yao na kutoa taarifa dhidi ya viendo vya ukatili wanavyotendewa alisema katibu tawala huyo".

Aidha amesema zoezi hilo la uundwaji wa mabaraza ya watoto kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa hiyo lishafanyika hivyo kuwahimiza wahusika kulifanyia kazi suala hilo huku akiwataka wazazi walezi na jamii nzima kupinga ukatili wa watoto unaoendelea katika maeneo mbali mbali.

Akisoma lisala ya maadhimisho hayo mbele ya mgeni rasmi mjumbe wa baraza la watoto Manispaa ya Bukoba Johnson Wilson iliyoandaliwa na afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Bukoba amesema kuwa Manispaa hiyo kwa kushirikiana na wadau wa mapambano dhidi ya ukatili na unyanyasaji wa  watoto wameweza kushughulikia na kutatua mashauri mbali mbali ya watoto yapatayo 269.

Mjumbe huyo ameongeza kuwa Manispaa hiyo kupitia mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) imeweza kuunda kamati za kuzuia ukatili kwa wanawake na watoto katika kata 14 za manispaa hiyo hatua iliyosaidia kupunguza vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa watoto kwa kiwango kikubwa.

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo " TUTEKELEZE  AJENDA YA 2040 KWA AFRIKA INAYOLINDA HAKI ZA MTOTO".

ikumbukwe kuwa juni 16 Kila mwaka bara la afirika huadhimisha siku ya mtoto wa afrika tangu kuidhinishwa kwa siku hiyo na umoja wa afrika mwaka 1991, ambapo umoja wa afrika ulianzisha siku hiyo Kama sehemu ya kuwakumbuka na kutambua mchango wa watoto waliopoteza maisha katika mauaji yaliyotokea huko Soweto,  Afrika ya kusini wakati wakidai haki zao za msingi.

No comments:

Post a Comment

Pages