HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 14, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza-Isaka Km 341 mkoani Mwanza

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiangalia Karatasi yenye majina ya viongozi mbalimbali walioshiriki kufanikisha kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitembea kwenye mfano wa Reli ya Kisasa itakayojengwa kutoka Mwanza hadi Isaka mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.

Wananchi wa Mkoa wa Mwanza waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo
mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021. PICHA NA IKULU.

 

No comments:

Post a Comment

Pages