June 21, 2021

RC KUNENGE AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA TATU AWATAKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO IPASAVYO


Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe Nikson Saimon akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani wa Pwani Aboubakar  Kunenge kushoto wakati wa halfa fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkoa wa Pwani na kuhudhulia na viongozi mbali mbali wa Serikali.

 

 NA VICTOR MASANGU, PWANI  

MKUU wa Mkoa wa Pwani Aboubakar  Kunenge amewaagiza wakuu wapya wa wilaya waliochaguliwa hivi karibuni kuhakikisha kwamba wanatimiza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kulivalia njuga suala la kukomesha na kutatua suala la  migogoro ya ardhi sambamba na kusimamia ipasavyo miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kuzingatai sheria na taratibu bila ya  kufanya uonevu wowote  kwa wananchi.

 Kauli hiyo ameitoa wakati wa halfa fupi ya kuwapisha wakuu wapya wa wilaya   mbali mbali za Mkoa wa Pwani  ambao wameteuliwa hivi karibuni na Rais wa  awamu  ya  sita  Samia  Suluhu  Hassan  kutoka , Wilaya za Mkuranga, Kisarawe, pamoja na  ,Kibiti na kuwataka kuweka mipango madhubuti  ya kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.

 

Pia  Kunenge  amewasisitiza  wakuu hao wa Wilaya kusimamia sheria asiwepo mtu wa kupendelewa wala atakayeonewa.

 

Aliwataka wakazi wa mkoa huo kuheshimu sheria huku akionya wenye tabia ya kuvamia maeneo na kuyauza kuacha tabia hiyo.

 

" Baadhi ya migogoro ipo katika maeneo ambayo yana hatimiliki za ardhi, kama shamba utaratibu upo utafuatwa na mamlaka zinazohusika" alisema.

 

Mkuu huyo pia  aliwawataka wakuu hao wa wilaya kutatua kero za wananchi ambazo zipo ndani ya uwezo wao na zilizo nje wahakikishe wanazifahamu kabla ya kuzifikisha mamlaka za juu.

 

"Kama kila mmoja atasimamia majukumu anayotakiwa hakutakuwa na kero kwa wananchi siamini katika uongozi wa mtu mmoja tushirikiane na kila mmoja awe tayari kujifunza" alisema.

 

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka kushirikiana na Halmashauri kuongeza mapato na kusimamia miradi ikamilike kwa wakati na kwamba  kila mmoja  asimamia uainishaji wa maeneo ya uwekezaji lakini pia maboresho ya madaftari ya makazi.

 

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe Niksoni Saimoni almaarufu niki wa Pili amesema kuwa atatekeleza maelekezo na  maagizo yote ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa na kwamba lengo lake kubwa ni  kutumia maarifa aliyonayo katika kuwaletea mabadiliko chanya wananchi pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbali mbali zilizopo katika sekta tofauti.

Kadhalika Mkuu huyo  alisema pamoja na nafasi aliyopewa mchango wake katika sanaa utaendelea kuwepo katika ajenda za kitaifa, Mkoa na Wilaya.

 

Naye Mkuu  mpya wa Wilaya ya Kibaha  Sara Msafiri amemshukuru Rais kwa kumumini  tena na kuahidi kushirikiana bega kwa began a wananchi wake katika kutatua kero na kwamba atatumia fursa ya viwanda vilivyopo katika kukuza uchumi na kuwapatia fursa ya ajira vijana ili kuweza kuleta chachu ya maendeleo na kuondokana na wimbi la umasikini

 

Pia  Sara Msafiri aliahidi kutekeleza maagizo ya mkuu wa Mkoa huku akisema ataanza kwa kukaa na wananchi kwenye maeneo ya migogoro kuitafutia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Pages