June 20, 2021

Sensa uso kwa uso na vyombo vya usafiri wa majini


Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa Dk. Albina Chuwa (kulia), akisaini
makubaliano kwa kushirikiana kufanya sensa ya vyombo vya usafiri majini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Kaimu Mkeyenge.


 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) kwa mara ya kwanza kufanya sensa kwenye usafiri wa vyombo vya majini.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini ya makubaliano kwa kushirikiana kufanya sensa ya vyombo vya usafiri majini
mtakwimu mkuu, ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa, amesema wapo tayari kutoaushirikiano katika kuhakikisha kwamba zoezi hilo linaenda vizuri.


"Naamini kwamba kila kitu kitaenda kwa mujibu wa taratibu na mikakati ya Serikali hivyo basi kila kitu kitakwenda sawa,” amesema  Dkt Chuwa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Mkeyenge, kwenye mkutano huo na waandishi wa habari amesema sense hiyo ya vyombo vya usafiri majini ni ya kwanza kufanyika nchini Tanzania .

“Kama ambavyo wengi wetu tunajua, vyombo vya usafiri majini hutumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kusafirisha abiria, mizigo, uvuvi, utalii na matumizi mengine katika maneneo mengi nchini,” amesema.

Aidha amesema kuwa, pamoja na mambo mengine, vyombo vya majini vina mchango mkubwa kiuchumi na pia huwezesha shughuli mbalimbali za kijamii.

Mkurugenzi mkuu huyo amesema ufanyaji wa sensa ya vyombo vya usafiri wa majini utakuwa na faida ikiwemo,kuandaa kanzidata (database) ya vyombo vya usafri nchini, ambayo itatumika katika kuboresha sera, mipango na usimamizi wa sheria, kanuni na maagizo ya kudhibiti mambo yanayohusu usalama wa usafiri majini.

Hata hivyo, ametaja faida nyingine ya sensa hiyo ya vyombo vya usafiri wa majini kuwa ni kusaidia katika ufuatiliaji (monitoring) wa matokeo ya utekelezaji wa sera au mipango mbalimbali.

“Pia hili zoezi litasaidia katika ukusanyaji wa takwimu na kuwezesha ufanyaji wa tafiti mbalimbali, kufanya maamuzi ya uwekezaji na biahara kuhusu vyombo vya usafiri majini na usafiri kwa njia ya maji kwa ujumla,” ameeleza


Na kuongeza kuwa "Sensa ya vyombo vya usafiri wa majini katika maeneno ya maji, kwa Tanzania bara, Tasac na NBS vimekubaliana kuendesha zoezi hilo na kwamba Tasac itatoa utaalamu unaohitajika wa masuala ya usafiri wa majini ili matokeo ya sensa yawe na thamani kwa watumiaji," amesema mkurigenzi Mkuu huyo.

No comments:

Post a Comment

Pages