June 18, 2021

TBS YAOKOA BILIONI 6.5 UWEKAJI WA VINASABA KWENYE MAFUTA

Mkuu wa Shughuli za Uwekaji Vinasaba Mhandisi Florian Batakanwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango (TBS) leo Jijini Dar es Salaam.

*********

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS),katika kipindi cha miezi miwili kasoro limefanikiwa kuweka vinasaba katika lita Milioni 464,215,825 za mafuta na shughuli ya kuweka vinasaba gharama yake kwa lita moja ni shilingi 14 hivyo mpaka sasa wameweza kuingiza fedha kiasi cha shilingi Bilioni 6.5 na fedha hiyo inaingia moja kwa moja serikalini.
 
Ameyasema hayo leo Mkuu wa Shughuli za Uwekaji Vinasaba Mhandisi Florian Batakanwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika la Viwango (TBS) leo Jijini Dar es Salaam.
 
Amesema shughuli ya kuweka vinasaba katika mafuta inawekwa kwenye maghara yanayopokea mafuta bandarini ambayo kwa Dar es Salaam kuna maghala 19 ambayo wamekabidhiwa na EWURA na mkoani kuna maghala matatu lakini pia kuna maghala mawili yameongezeka hapa jijini na kufanya kufikia 21 kwa Dar es Salaam.
 
"Zoezi hili mwanzo lilikuwa linafanywa na taasisi isiyo ya kiserikali hivyo mapato yote haya yalikuwa yanaenda kwenye taasisi hiyo na serikali ilikuwa inapata kodi kwenye taasisi hiyo'. Amesema Mhandisi Batakanwa.
 
Aidha Mhandisi Batakanwa amesema hii zoezi la kuweka vinasaba kwenye mafuta lina uhusiano mkubwa na usalama wa nchi kwani mtu ama kampuni binafsi akiweza kugawa vinasaba kwa watu wasiohusika nchi inakuwa inateteleka kwasababu kiuchumi inakosa mapato yake.

No comments:

Post a Comment

Pages