June 07, 2021

WAJASIRIAMALI, WAFANYABIASHARA ANZENI KUTUMIA MISIMBOMILIA KWENYE BIDHAA MNAZOZALISHA

 


 Washiriki wa mafunzo hayo ya wajasiriamali wa makampuni mbalimbali yalioalikwa kushiriki mafunzo hayo wakifuatilia maelezo kutoka kwa Meneja wa Sido Mkoa wa Arusha Nina Nchimbi juu ya umuhimu wa kuzalisha bidhaa zao kwa ubora unaokubalika kwenye masoko ya kimataifa kama
walivyokutwa na kamera ya Matukio mapema leo kwenye ukumbi wa ofisi yaMkuu wa mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.



Na Ahmed Mamoud, Arusha
 

Wajasiriamali Kote nchini wameaswa kujiunga program ya Msimbomilia (Barcorde)unaotambulika kimataifa utakaowasaidia bidhaa zao kutambulika kwenye masoko ya kimataifa ya ndani na njee ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Dkt.Athman Kihamia wakati akizindua mpango wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo
wajasiriamali na wafanyabiashara wa mkoa huo juu ya umuhimu na matumizi ya msimbomilia Barcordes na ufuatiliaji wa mfumo wa ufuatiliki na viwango yaliondaliwa na kampuni ya Global Standard one
(GS1) iliyofanyika jijini Arusha.

Alisema kuwa alama hizi za mistari yaani Msimbomilia ni muhimu sana kwenye Mnyororo wa Ugavi ambao unahusisha wazalishaji wa bidhaa kwenye kubadilishana taarifa kwa bidhaa kwani zisizo na Barcorde zinakosa sifa ya kuingia kwenye Mnyororo wa Ugavi hivyo kumsababishia mzalishaji kutofikia viwango hivyo kupungua kwa mauzo yake sokoni.

Dkt. Kihamia alisisitiza kuwa uzalishaji unaoenda sambamba na matumizi bora ya Tehama utasaidia kuongeza ubora wa bidhaa zetu zinazozalishwa
na wakulima hapa nchini hivyo kusaidia kuingia kwenye masoko ya kimataifa ya ndani na njee ya nchi na kufikia kwenye maendeleo ya kweli yatakayosaidia kuongeza uzalishaji wenye tija.

"Wajasiriamali nendeni mkasome Sido na Veta kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa bidhaa zenu ili kupata usajili wa Tbs bure na serikali yenu imeona umuhimu huo wa kupata huduma za msimbomilia kwa bei ya offer utakaongeza uzalishaji wenye ubora kwenye masoko ya kimataifa ya ndani na nje ya nchi"

Aidha kutokana na serikali kuona changamoto hizo kwa maksudi na nia thabiti ya kuisaidia jamii ya wajasiriamali,wafanyabiashara na sekta binafsi iliamua kushiriki mchakato wa kuanzishwa kwa taasisi ya ufuatiliaji katika bidhaa zinazozalishwa nchini na nje ya nchi uanachama katika shirika la GS1 Global ambalo lina hatimiliki ya huduma kadhaa ikiwemo Msimbomilia.

Kwa Upande wake Mkuu wa Masoko wa kampuni ya GS1  hapa nchini Eric Kafula alisema kuwa katika kusherehekea miaka kumi ya shirika hilo wao
na serikali kupitia Tamisemi wameandaa mafunzo hayo kwa mikoa 10 hapa nchini juu ya umuhimu wa kuwa na Misimbomilia kwenye bidhaa za
wajasiriamali na mkoa wa Arusha umepewa kipaumbele baada ya kugundua ni mji wa kitalii una fursa nyini za kibiashara na wengi wanahitaji
kuwa na masoki ya uhakika.

Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 barani Afrika ambazo bidhaa zao zinatumia huduma ya Misimbomilia na hivyo kuongeza utambuzi
wa ubora wa bidhaa zake kwenye masoko ya kimataifa na kuwataka wajasiriamali kwenda kusoma Sido na Veta ili waweze kupata nembo ya
TBS bure kwani gharama za usajili kwa wajasiriamali ni kubwa hivyo watumie fursa hiyo ya serikali yetu.

"Kwenye mafunzo ya kusherehekea miaka 10 ya kuanzishwa Taasisi yetu ya GS1 tumetoa offer ya ujisajili wa huduma ya Misimbomilia kwa nusu bei
kwa wajasiriamali wote watakaoshiriki mafunzo yetu kwani pamoja na bidhaa nyingi kuzalishwa na kukosa utambuzi wa mifumo ya kimataifa ya
Tehama lakini pia kulikuwa na changamoto katika uchumi wa nchi kwa wazalishaji wengi na wafungashaju kushindwa kupata huduma hii kwenye
bidhaa zao "

Nae Meneja wa Sido mkoani Hapa Nina Nchimbi alisema serikali kwa kuona umuhimu wa uzalishaji wa bidhaa zenye ubora ndio maana wakaja na
mafunzo maalum yanayotolewa na taasisi zetu za Sido na veta ili wajasiriamali waweze kupata nembo ya TBS bure ndani ya miaka mitatu
kuanzia sasa.

"Niwaombe ndugu zangu wajasiriamali tumieni fursa hii ya kuongeza ubora wa bidhaa zenu kuja kupata Elimu na mafunzo ya uzalishaji wenye tija kwetu utakaosaidia kupata TBS bure na hivyo kuongeza mnyororo wa Ugavi na kuyafikia masoko ya kimataifa"

No comments:

Post a Comment

Pages