June 02, 2021

WASHIRIRIKI JUMA LA ELIMU WAENDESHA MIJADALA YA ELIMU NAKUHAMASISHA JAMII

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng'ong'a (kushoto) walioshika chepe wakiwaongoza wadau wa TEN/MET Shule ya Msingi Obwere kukishiriki katika shughuli za nguvu kazi kwenye ujenzi wa madarasa shuleni hapo ikiwa ni kuhamasisha wana jamii kushiriki moja kwa moja ujenzi wa miundombinu ya elimu.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Rorya, Gerald Ng'ong'a (kushoto) walioshika chepe wakiwaongoza wadau wa TEN/MET Shule ya Msingi Obwere kukishiriki katika shughuli za nguvu kazi kwenye ujenzi wa madarasa shuleni hapo ikiwa ni kuhamasisha wana jamii kushiriki moja kwa moja ujenzi wa miundombinu ya elimu.




Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (kushoto) akizungumza na wanafunzi, wazazi, walimu, viongozi anuai na wadau wa elimu Sekondari ya Profesa Philemon Sarungi ikiwa ni kushirikishana fursa na changamoto zilizopo katika elimu kwenye maeneo yao na namna ya kuzitatua kuanzia ngazi ya jamii.

Wanafunzi Shule ya Sekondari Profesa Philemon Sarungi wakishiriki katika mijadala hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja Nyalandu (kushoto) akizungumza na wanafunzi, wazazi, walimu, viongozi anuai na wadau wa elimu Sekondari ya Profesa Philemon Sarungi ikiwa ni kushirikishana fursa na changamoto zilizopo katika elimu kwenye maeneo yao na namna ya kuzitatua kuanzia ngazi ya jamii.

Mikutano na mijadala ikiendelea na makundi mbalimbali kushirikishana changamoto.

Mikutano na mijadala ikiendelea na makundi mbalimbali kushirikishana changamoto.

Mikutano na mijadala na wanafunzi ikiendelea kushirikishana utatuzi wa changamoto za elimu.

Mikutano na mijadala na walimu ikiendelea kushirikishana mbinu za utatuzi wa changamoto za elimu.

Mikutano na mijadala na walimu ikiendelea kushirikishana utatuzi wa changamoto za elimu.

Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za nguvu kazi.


Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za ujenzi kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.


Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za ujenzi kwa kufyatua tofali kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.

Wanachama wa Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), wakishiriki katika shughuli za ujenzi kwa kufyatua tofali kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.





Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Maadhimisho  ya Juma la Elimu  Kitaifa Greison Mgoi akishiriki katika shughuli za ujenzi kuhamasisha jamii kushiriki ujenzi miudombinu ya elimu.


Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga (katikati) akishiriki shughuli za ujenzi katika maadhimisho juma la elimu.


Na Mwandishi Wetu, Rorya

WANACHAMA wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) leo wameanza kufanya mikutano na wazazi, wanafunzi, walimu na pamoja na viongozi huku wakishiriki katika shughuli za nguvu kazi kwenye ujenzi wa madarasa ikiwa ni kuhamasisha wana jamii kushiriki moja kwa moja ujenzi wa miundombinu hiyo ya elimu.

Wakishirikiana na viongozi wa elimu kuanzia ngazi ya kata hadi Wilaya ya Rorya wamefanya shughuli hizo katika Shule ya Msingi Obwere pamoja na Sekondari ya Profesa Philemon Sarungi ikiwa ni kushirikishana fursa na changamoto zilizooo katika elimu kwenye maeneo yao na namna ya kuzitatua kuanzia ngazi ya jamii yenyewe.

Akizungumza na wanajamii katika mikutano hiyo, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga  alisema utatuzi wa changamoto zilizopo katika elimu unaanzia katika ngazi ya jamii kwa kushirikishana kwenye mijadala kabla ya kuanga kupanda ngazi za juu. 

Bw. Wayoga alisema mikutano na mijadala inayofanyika ni mwendelezo wa shughuli za Maadhimisho ya Juma la elimu ambazo kitaifa zinafanyika wilayani Rorya. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni; Uwekezaji katika mifumo ya Elimu kwa malengo ya maendeleo endelevu (Financing Education System for Sustainable Development Goals), kauli inayoikumbusha jamii umuhimu wa juhudi ya pamoja kama wadau wa elimu, yaani serikali, Asasi za Kiraia, sekta binafsi, wanafunzi, wazazi na wananchi kwa ujumla. 

Miongoni mwa mashirika wanachama na wadau walioshiriki katika shughuli za leo ni pamoja na PCI, Uwezo Tanzania, Haki Elimu, ADD International, Shule Direct, Sense International, Child Support Tanzania, Malala Foundation, Right to Play, RELI Tanzania, CAMFED, WeWorld, Pestalozzi Children’s Foundation, OCODE, PWC, SAZANI TRUST-ZANZIBAR, SAWO na TEN/MET Secretariat.

Mikutano na mijadala na walimu ikiendelea kushirikishana utatuzi wa changamoto za elimu.

No comments:

Post a Comment

Pages