June 21, 2021

WASHONAJI VIKAPU NJOMBE WAIOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA SOKO LA UHAKIKA

 

  

Wakazi wa Kijiji cha Ikando mkoani Njombe wakikata nyasi kwa ajili ya kwenda kutengenezea vikapu. (Picha na John Dande).

  

Wakazi wa Kijiji cha Ikando mkoani Njombe wakiandaa nyasi kwa ajili ya kushonea vikapu. 


Mkazi wa Kijiji cha Ikando Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Maria Muhema, akishona moja ya kikapu kwa ajili ya kuweza kuviuza. 

  
Mkazi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe, Furaha Kilasi, akishona moja ya kikapu kwa ajili ya kuweza kuviuza kujipatia riziki.


Picha ya pamoja baada ya kumaliza kushona vikapu hivyo.

 

Na Mwandishi Wetu, Njombe

 

Washonaji wa vikapu Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe wameiomba serikali kuwatafutia soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao za vikapu ili kuweza kuleta tija.

Wakizungumza na waandishi wa habari washonaji hao wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kukosa soko la uhakika na hivyo kulazimika kuuza bila ya faida.

Mmoja wa washonaji hao akiwemo Maria Muhema (61) mama wa watoto watano mkazi wa kijiji cha Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe,amesema ameanza kazi ya ushonaji vikapu tangu akiwa msichana ili kujipatia kipato lakini soko hilo limekua likizunguuka maeneo yao tu hivyo kushindwa kunufaika kwa sababu ya kuuza kwa mazoea.

“Elimu ya ushonaji vikapu tulifundishwa na mzungu alitokea Njombe mjini na nilianza  tangu nikiwa msichana kipato chake bado ni kidogo,lakini ninavyofikiri tukipata mateja nje ya mkoa wetu tutanyanyuka kiuchumi”amesema Maria.

Alisema kuwa wateja wapo lakini bado malighafi za kutengenezea bidhaa hizo kama nyasi  zimekua changamoto kupatikana.

“Kutengeneza hivi vikapu tunatumia nyasi ambazo zinaota kando ya mto lakini wakati mwengine zinakua mbali hivyo tunalazimika kununua kwa vijana ambao wanatuuzia shilingi 10,000 ambapo ukilinganisha na uuzwaji wake wa kusuasua tunapata hasara”amesema.

Naye Furaha Kilasi (39) mkazi wa kijiji cha Ibumila hlamshauri ya wilaya ya Njombe ni mama watoto watatu amesema suluhisho la bidhaa hiyo kuwa na thamani ni kutafuta soko la nje kwa sababu la ndani halijabadilisha maisha yao.

“Nina watoto ninasomesha kupitia kazi hii lakini tunapata kidogo sana,tunaamini tukipata soko la nje bei ya kikapu itaongezeka….ugumu wa maisha ndio ulionifanya nishone vikapu lakini sasa bei haiendani na uandaaji wake ambapo kikapu kinaanzia shilingi 4000 hii sio nzuri kwetu”amesema Kilasi.

Kwa upande wa Sayuni Kaduma (26) mkazi wa kijiji cha Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe,mama wa mtoto mmoja alianza kushona vikapu tangu akiwa mtoto amesema soko la vikapu sio rafiki kwa sababu bei zake ziko tofauti.

“kwa siku tunashona vikapu kimoja au viwili,bei ziko tofauti soko sio zuri unakuta mteja anakuagiza bidhaa ukimpelekea anaanza kujishushia bei au anakwambia havina ubora wakati huo sapo ulishamtumia pamoja na bei zake”amesema Sayuni.

Pia Sayuni ameiomba serikali kuwaunga mkono kwa kuitambua bidhaa hiyo kwa kuwatafutia soko la nje pamoja na kuwatambua katika mikopo ya halmashauri ya asilimia tano za wanawake.

No comments:

Post a Comment

Pages