Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Gerad Mweli, akizungumza na Maafisa elimu wa mikoa maafisa elimu taaluma wa mikoa pamoja na Maafisa elimu msingi wa halmashauri wakati wa kufunga mafunzo ya uthibiti ubora wa elimu.
Mtendaji mkuu wa Adem Dr. Dustin Mgullah akitoa taarifa kwa Mgeni rasmi kuhusiana na mafunzo ya uthibiti ubora wa elimu ambayo yalifanyika Wilayani Bagamoyo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo ya uthibiti ubora wakiwa katika ukumbi huo wa Adem. (Picha na Victor Masangu).
Na Victor Masangu, Bagamoyo
Naibu
katibu mkuu Ofisi ya Rais Gerad Mweli amewagiza maafisa elimu wa mikoa
pamoja na wakurugenzi nchi nzima kuhakikisha kwamba wanaanza Mara moja
ujenzi wa miradi ya madarasa kwani fedha zake zimeshatolewa na serikali
katika kuboresha sekta ya elimu.
Mweli
aliyasema hayo wakati wa kufunga rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo
katika suala la uthibiti ubora wa elimu kwa maafisa elimu wa mkoa nchi
nzima,maafisa taaluma wa mikoa pamoja na Maafisa elimu msingi wa
halmashauri yaliyofanyika katika ukumbi wa Adem Wilayani Bagamoyo
Aidha
aliwataka kuhakikisha kwamba wanakwenda kuyatumia vizuri mafunzo hayo
waliyopatiwa kwa ajili ya kuthibiti ubora wa elimu na kuweka mikakati
mathubuti ambayo itaweza kusaidia kuinua kiwango Cha elimu hapa nchini.
Naibu
katibu mkuu huyu alisema lengo la serikali ni kuboreha sekta ya elimu
hapa nchini hivyo maafisa elimu hao pamoja na Maafisa taaluma wanapaswa
kusimamia ipasavyo fedha zote ambazo zinatolewa na serikali katika
kutekeleza miradi mbali.mbali ya elimu.
Aliongeza
kuwa anasikitishwa Sana kuona Hadi Sasa Kuna baadhi ya halmashauri
nchini zimepatiwa fedha lakini zimeshindwa kuanza kabisa ujenzi wa
madarasa ambapo ameahidi kulivalia njuga suala Hilo.
'Kwa
kweli katika Jambo hili siwezi kumvumilia mtu yoyote hata tunatakiwa
tufanye kazi maana Mimi nimepokea mezani kwangu halmashauri zipatazo ,60
serikali imezipatia fedha lakini cha kushangaza bado haziaanza kabisa
ujenzi wa madarasa kwa kweli hili Jambo siwezi kulifumbia macho,'alisema
Kadhalika
aliwakumbusha maafisa elimu hao kutumiza wajibu wao ipasavyo na kuwema
mipango madhubuti katika kuboresha miundonbinu ya madarasa kwani Kuna
maeneo mengine madarasa bado ni chakavu.
Katika
hatua nyingine aliupongeza uongozi wa Adem kwa kuweza kutoa mafunzo
hayo ya siku nne kwa maafisa elimu hao ambayo yatawasaidia katika
kuongeza Chachu zaidi katika suala la usimamizi wa elimu hapa nchini.
Kwa
upande wake mtendaji mkuu wa Adem Dr.Siston Mgullah amebainisha kuwa
lengi kubwa la kufanyika kwa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maafisa
elimu hao katika suala zima la uthibiti ubora wa elimu.
Pia
aliongeza kuwa mafunzo hayo ambayo yamewashirikisha jumla ya washiriki
wapatao 232 yataweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya elimu
kutoka na mada mbali.mbali ambazo zimetolewa hivyo ana Imani maafisa
elimu hao wataweza kuleta matokeo chanya.
Katika
hatua nyingine alisema kuwa Adem itaendelea kushirikiana na serikali
bega kwa bega katika kuwapatia ujuzi wa Mara kwa Mara maafisa elimu wote
katika ngazi mbali mbali hapa nchini lengo ikiwa ni kusaidia kuboresha
elimu.
Kadhalika aliiomba
serikali kuwapa kibali Cha kwenda kutembelea katika shule mbali mbali
ili kujionea mafanikio ambayo yametokana na mafunzo hayo na kwamba lengo
lao kubwa ni kuona kunakuwa na mabadiliko chanya katika elimu.
No comments:
Post a Comment