Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
WAUGUZI wanaofanya kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),wameshauriwa kuwa wavumilivu, kuwaheshimu wakubwa wao na kupendana wenyewe ili kuleta ufanisi katika kazi zao.
Hayo yalisema jijini Dar es Salaam jana na Msataafu katika nafasi ya muhudumu wa afya Devota Mhando kwenye sherehe ya kuagwa kwao iliyoandaliwa na Wauguzi wa hospitali hiyo alisema alifanya kazi miaka 41 hospitalini hapo.
Alisema kuwa alianza kazi katika hospitali hiyo tangu mwaka 1980 akiwa na umri wa miaka 21 na hajawahi kusimamishwa wala kufukuzwa kazi.
Devota aliongeza kwa katika kipindi cha miaka 41 aliyofanyakazi Muhimbili kulikuwa na changamoto nyingi lakini aliweza kuvumilia hadi anastaafu kwa mujibu wa kanuni na sheria ya nchi.
"Muhimbili ndio Hospitali yangu ya kwanza kuanza kufanya kazi hadi nafikia umri wa kustaafu, sijawahi kusimamishwa wala kufukuzwa kazini ngao yangu kubwa ilikuwa ni uvumilivu," alisema Devota.
Alieleza kuwa kuwa matarajio take ni kuungana na mume wake katika ujasirimali wa kutengeneza majiko sanifu na kuyasambaza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Sebastian Luziga alisema kuwa wamejifunza mambo mengi kupitia wastaafu wawili waliowaaga yakiwamu uvumilivu kazini na kutimiza wajibu wao kwa wakati.
"Tulichojifunza kutoka kwa wastaafu hawa ni kutimiza miaka 60 wamepita katika changamoto nyingi na vikwazo walivyopitia hadi kufikia hatua ya kustaafu," alisema Luziga.
Aliongeza kuwa hiyo ni safari ndefu sio wote wanaweza kufikia umri wa kustaafu na kwamba aliwatakia kila la heri katika maisha yao mapya.
No comments:
Post a Comment