June 30, 2021

Wizara ya Ardhi yatoa hati za viwanja katika Maonyesho ikiwamo ya mke na mume


Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa
Kayera (kushoto), akiwakabidhi hati ya kiwanja wakazi wa Kivule Samweli Mwakatage na mkewe Tatu Salehe katika banda la Wizara ya Ardhi Nyumbai na Maendeleo ya Makazi.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

WIZARA ya Ardhi, Nyumbai na Maendeleo ya Makazi, imewataka wananchi kutembelea banda la Wizara hiyo katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ( saba saba), ili kuweza kuhudumiwa kwa haraka na kwa muda mfupi.

Haya yamesemwa na Kamishna wa  Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam, Idrisa Kayera  katika banda  hilo  wakati akiwakabidhi hati ya kiwanja wakazi wa Kivule jijini hapa Samweli Mwakatage na mkewe Tatu Salehe, amesema wananchi wameshaanza kupata uelewa.

Kamishna huyo amesema Wizara hiyo tayari imeshakabidhi hati za vipande vya ardhi ama viwanja zaidi ya 40 jana na leo.

Anafafanua kuwa siku ya kwanza wamekabidhi hati 30 ikiwamo ya mke na mume na kwamba siku ya pili pia  wamekabidhi hati hizo za viwanja 11.

Amesema Waziri wa Ardhi William Lukuvi alishatoa tangazo kuwasisitiza wananchi kumiliki kipande cha ardhi kama mke na mume.

" Hii inaondoa migogoro ambayo inatokea kwenye masuala ya mirathi pale mmoja anapofariki dunia i na atakayebaki ataendelea kumiliki kipande cha ardhi ," amesema.

Ameongeza kuwa ushiriki wao katika maonyesho hayo ya mwaka huu wamejipanga vizuri na kwamba huduma zilizokuwa zikitolewa wizarani zinatolewa kwa haraka zaidi na kwa muda mfupi kwenye banda hilo.

" Hadi muda huu wa saa nane mchana tangu tulivyoanza asubuhi kutoa huduma zetu tayari tumeshatoa hati  11 siku ya kwanza tumekabidhi hati 30 ikiwamo ya mke na mume, " ameeleza.Kayera.

Mara baada ya kukabidhiwa hati Mwakatage amesema hakuna urasimu katika upatikanaji wa hati hiyo na kwamba tangu alipofanya malipo imechukua muda wa wiki mbili tu kuipata hati hiyo..

" Tangu nilipofika katika banda hilo haichukua nusu saa tayari nakabidhiwa hati yetu nina furaha sana nawaasa wanaume wenzangu wawashirikishe wake zao mambo ambayo wanayafanya " amesema.

Ameongeza kuwa hati hiyo ataitumia katika mambo ya kimaendeleo ikiwamo kuombea mikopp kwenye taasisi za kifedha.

Kwa upande wake Tatu ametoa wito kwa wanaume wengine kuwashirikisha wake zao katika mambo wanayoyafanya na wasitumie mabavu ya kigezo cha kuwa wao ndio vichwa vya familia.

No comments:

Post a Comment

Pages