MkurugenziI Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), William Erio akielekeza jambo waandishi wa habari.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), William Erio amesema udhibiti wa bidhaa bandia nchini umekuwa mgumu kutokana na mabadiliko ya teknolojia jambo ambalo limefanya ugunduzi wake kuwa shida
Pia amesema wanatarajia kufungua ofisi za kanda za tume hiyo katika sehemu zote za mipaka ambayo bidhaa hupitishwa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti uingizwaji bidhaa bandia.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mwananchi katika maonyesho ya 45 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) ambayo yalianza Juni 28, 2021 na yanatarajiwa kukamlika Julai 13 mwaka huu
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa pamoja na changamoto hiyo wakati mwingine mtu huweza kuibaini kutokana na ufungashaji wake, bidhaa haikufungashwa vizuri, haina nembo ya mzalishaji wala muda wa matumizi
Amesema wamejipanga kuwashughulika na wanaoleta bidhaa bandia nchini ambazo baadhi hudhibitiwa na nyingine kuingia nchini na kwamba watambua kuwa FCC watahakikisha kuwa hilo linadhibitiwa
“Kwa sasa tuna ofisi Dar na Dodoma lakini tunatarajia tutafungua ofisi za kanda ikiwemo Mbeya ambapo tutadhibitu mipaka yote ambayo hutumika kuingia nchini," amesrma Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa watakuwa na ofisi katika sehemu ambazo bidhaa huingilia nchi kavu au majin na kwamba Hilo watalifanya ili kuhakikisha linakwenda vizuri.
Erio amesena suala la vita ya kupambana na bidhaa bandia lisiachwe kwa FCC pekee bali Wananchi nao inabidi washiriki katika vita hiyo kwani uwepo wao unachangia ukwepaji kodi
Amesema wapo baadhi ya watu wanazipenda bidhaa zinazouzwa kwa bei Bidhaa nafuu ambazo ni bandia kwa kusema zinaendana na hali ya maisha yao bila kujali kwa kufanya hivyo kunawezesha wauzaji kukwepa kulipa kodi.
"Watu ni lazima watambue kuwa ni gharama nafuu na ni hatarishi, hebu fikiria umetumia dawa bandia au umejenga nyumba yako kwa gharama kubwa halafu unatumia nyaya za umeme za bandia,” amesema Erio
Pia amezungumzia kuhusu
kampuni kuungana amesema
Kwa mujibu wa sheria kampuni zinazotaka kuungana zinatakiwa kupeleka maombi FCC na endapo yataridhiwa kuwa na matokeo chanya itakubaliwa
Mkurugenzi huyo ameleza kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia uzalishaji wa bidhaa bora kwa ajili ya ushindani masokoni ikiwemo lile la Jumuiya ya Afrika mashariki lililofunguliwa na soko la bidhaa la Afrika linakaribiia kufunguliwa
Ameongeza kuwa wao wamejipanga kuhakikisha kuwa wanashughulikia maombi haya kwa haraka na siku chache zilizopita walifanya kikao kwa mara ya kwanza walipokea maombia 19 ndani ya siku moja.
Aidha amezitaka kampuni ambazo zinataka kuungana na zile za nje ili kuimarisha uzalishaji kuzingatia sheria na zilizowekwa.
No comments:
Post a Comment