July 02, 2021

Maadhimisho ya siku ya mwanamke mwenye ulemavu yapigiwa chapuo

 
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

 

NAIBU Spika Dk.Tulia Ackson amewataka wabunge kuunga mkono hoja ya Tanzania kuwa na maadhimisho ya siku ya mwanamke mwenye ulemavu pindi itakapoletwa bungeni.


Aidha, amesema uwepo wa siku hiyo utasaidia kuwepo kwa wigo mpana wa kujadili changamoto nyingi zinazowakabili wanawake wenye ulemavu tofauti na makundi mengine.

Dk. Tulia aliyasaema hayo juzi jijini Dodoma kwenye kikao baina ya wabunge na wadau mbalimbali wa masuala ya ulemavu kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund.

Alisema uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu itatoa nafasi kama taifa kujadili kwa upana changamoto zinazo wakabili.

“Siku hii ni muhimu sana kwani mwanamke mwenye ulemavu anakabiliwa na changamoto nyingi sana tofauti na makaundi mengine”alisema

Aliwataka wabunge kuhakikisha kuwa hoja hiyo iatakaletwa bungeni wanaiunga mkono kwa asilimia 100, ili bunge liweze kuridhia.

“Ili hoja yako ipite ni lazima waheshiwa wabunge waiinge mkono hivyo basi natumaini wabunge mmetuelewa sisi wanawake wenye ulemavu na hoja hii ikija bungeni mtaiiunga mkono kwa asilimia 100” alisema Dk.Tulia

Mwenyekiti wa Ikupa Trust Fund, Amon Mpanju alisema kuwa uwepo wa siku hiyo utatoa fursa kwa wanawake wenye ulemavu kujadiliakwa kina kero zinazao wakabili.

Alisema kama Bunge litaridhia uwepo wa siku hiyo basi Tanazania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na maadhimisho ya siku maalumu ya mwanamke mwenye ulemavu.

“Hii hoja siyo yetu pekee yetu hata wenzetu wa shirika la kimataifa la Un Woman pamoja na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA wamenaunga makono sisi kuwa na siku hii rasmi”alisema Mpanju

Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweze Idan Eyakuze, alisema takwimu zinaonyesha kuwa mwanamke mwenye ulemavu anakabiliwa na changamoto mara mbili zaidi ya yule asiye na ulemavu.

Pia, alisema wanawake wenye ulemavu wapo katika hatari ya kukumbana na ukatili kwa asilimia kubwa tofauti na wale wengine.

“Mwanawake wenye ulemavu yupo hatarini kukumbana na changamoto ya ukatili mara tano ukilinganisha na wale wasio na ulemavu”alisema

Kwa upande wake Mbunge Stellah Ikupa, alisema kuwa ipo haja kwa jamii kupata elimu ili kubadili mitazao juu ya watu wenye ulemavu.

“Tukipata siku hii itasadia ujadili chanamoto zetu hivi sasa sisi tunakabiliwa pia na changamoto ya kupendwa na kuwa na familia mlemavu kuolewa imekuwa ni kazi hasa sisi wanawake”alisema Ikupa.

No comments:

Post a Comment

Pages