Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021 umeongezeka hadi kufikia asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka iliridhia mwezi Mei, 2021.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii, Rith Minja amesema hiyo inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2021.
Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021, kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula.
"baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfuniko wa bei mojamoja na Vitambaa vya nguo kwa asilimia 8.5,nguo za wanawake kwa asilimia 6.3 viatu vya wanawake kwa asilimia 6.2,kodi ya panga kwa asilimia 4.9,vyakula kwenye mgahawa kwa asilimia 5.6 na gharama za malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7," alisema Minja.
Aidha amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021 umepungua hadi asilimia 4.7 kutoka asilimia 4.9 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2021.
Minja amesema nchini nchini Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021 umeongezeka hadi asilimia 6.32 kutoka asilimia 5.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei ,2021.
Hata hivyo amesema kwa upande wa nchi ya Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2021umeongezeka hadi asilimia 2.0 kutoka asilimia 1.9 kwa ulioishi mwezi Mei, 2021.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi Daniel Masolwa alisema amesema ofisi ya Takwimu katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya Takwimu Sura 351 itaanza kutangaza kwenye Tovuti yake viashiria vya kiuchumi kwa kipindi cha kila mwezi na na kila roba mwaka kuanzia mwezi Julai 2021
Alisema viashiria hivyo pammoja na vilivyokuwa vinatayarishwa na kusambazwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ambavyo ni wa bei kwa kila mwizi na pato la Taifa kwa kila robo mwaka.
"Viashiria vipya vitakavyoanza kusambazwa kwenye tofauti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu mojamoja na Uzalishaji wa Umeme, Uzallshaji wa Saruji, Idadi ya watalii wanaoingia nchini ( na baadaye zitatolewa kwa nchi wanaotoka) na Fahirisi ya uzalishaji wa vifaa vya ujenzi nchini, " amesema Masolwa.
Masolwa amesema viashiria hivyo ni muhimu katika kufanya tathmini na uwakilishi wa shughuli mbalimbali za uchumi katika kipindi cha muda mfupi wa kila mwezi na kila robo mwaka.
No comments:
Post a Comment