Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), Mhandisi Charles Sangweni akizungumza na waandishi wa habari.
Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema bado kuna changamoto ya nafasi muhumu za utafutaji mafuta na gesi asilia ambazo zinashikiliwa na wageni.
Mhandisi Sangweni amesema nafasi ya mtu anayesimamia uchimbaji ,anayeongoza kila kitu hakuna Mtanzania hata mmoja anayeshika nafasi hiyo.
Akizungumza jana katika banda lao la maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendele kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Vijana na Biashara Endelevu'
Amesema wana mfano miwili kipindi cha nyuma walichimba visima waliokuwa na wafanya ndani ya meli kama 160 lakini Watanzania walikuwa wanane tu.
" Tulipofika wakaimarisha mwaka 2018 tulichimba kisima kilichokuwa kimepewa jina la Pilibpili One tulikuwa Watanzania 58, naamini leo hii ikitokea kazi yoyote Watanzania wataongeza," amesema Mhandisi huyo.
Mhandisi Sangweni ameongeza kuwa kwa sasa wanashughuli zinazoendelea maeneo ya Ruvu na kwamba wanatimu ya watu zaidi ya 300 lakini changamoto iliyopo ni moja ya zile nafasi muhimu bado zinashikiliwa na wageni.
Amesema wanajua kwamba muda unavyoendelea Watanzania Wanazidi kujifunza kupitia wageni hao na mwisho wa siku watapata wenye nafasi hiyo.
Mhandisi huyo amesema fursa zilizopo kwenye mkondo wa juu wao ndio wanasimamia na kwamba Kuna sheria, miongozo, kanuni lakini hazitoshi kama hawataungana na yule anayesimamia.
Ameongeza kuwa rasilimali za hapa nchini ni za Watanzania na katiba imeelekeza wazi rasilimali yoyote ni ya mtanzania alieelewa haki yake ni kumiliki ardhi.
Mhandisi huyo ameeleza kuwa kwenye shushuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia wanapokuwa na uchimbaji wa visima wanakuwa na fursa nyingi kama vile za chakula, usafirishaji, mawasiliano ni sehemu ambayo hata mtu binafisi asiye na kampuni anapata fursa hiyo..
Katika hatua nyingine mahandisi huyo amesema hadi sasa Mamlaka yao imeingia mikataba takribani Makampuni 11 kati ya hayo Makampuni matatu yapo katika uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.
Pia amesema katika Makampuni hayo 11 kampuni moja ni la wazawa wa ya kitanzania ambao yanawekeza katika uzalishaji wa sekta hiyo ya mafuta na gesi asilia.
Mhandisi Sangweni amesema mwaka 2010,Pura ilifikia hadi Makampuni 27 lakini ilipofika mwaka 2014 bei ya mafuta ilishuka sana huku Makampuni mengi yaliondoka.
Ameeleza kuwa kila mkataba unaoingia na PURA, ni lazima TPDC iipitie kwani ni mbia hivyo uzawa wao unadhibitisha kupitia TPDC.
No comments:
Post a Comment