Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
TAASISI ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeanzisha utoaji wa huduma ya kuleta nafuu kwa haraka kwa wagonjwa wanaopata kiharusi na kuwahishwa kwenye huduma katika taasisi hiyo ndani ya saa sita hadi 12.
Akizunguma katika banda la taasisi hiyo kwenye maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), Muuguzi katika chumba cha upasuaji kutoka katika taasisi hiyo, Juma Rehani, amesema ndani ya saa hizo sita hadi 12 mgonjwa wa aina hiyo akiwahishwa kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa katika taasisi hiyo anaweza kupata nafuu na kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Na siyo tu kwenye ubongo, pia kwenye uti wa mgongo na sehemu mbalimbali za mwili. Wagonjwa waliopata kiharusi, ndani ya masaa sita mpaka 12 wakifika kwenye huduma hii anaweza akapata nafuu na akarudi kwenye hali yake ya kawaida,”amesema Rehani.
Amesema huduma hiyo ya tiba ni mpya na imeanza tangu Januari mwaka huu na hutolewa bila kupasua kwenye eneo la mwili ambalo linakuwa limeganda damu badala yake hutumia tundu dogo kupitia sehemu ya nyonga kuingiza mpira.
Amesema huduma hiyo inahusika zaidi na wagonjwa ambao wamepata matatizo ya kwenye mishipa ya damu iliyopo kwenye ubongo.
“Katika ubongo kuna mzunguko wa mishipa ya damu ambayo ikitokea ikipata hitilafu na damu ikaganda, na inapoganda kwa kutumia upasuaji wa kawaida, huwezi kutoa tone la damu lililoganda, kwa hiyo njia ya kisasa ambayo inatumika ni kutumia mipira kupitia kwenye nyonga kupitia mshipa mkubwa ambao unapeleka mpaka kwenye ubongo,”amesema Rehani.
“Kuna wale wagonjwa ambao wanakuwa wamepata kitu kinaitwa kiharusi ambao damu imevilia kwenye ubongo ambao katika kupitia mashine ya kisasa ambayo kwa Afrika Mashariki na Afrika ya Kati inapatikana MOI peke yake, ina uwezo mkubwa sana wa kufanya uchunguzi pamoja na matibabu kwenye mishipa ya damu.”
Amesema tangu huduma hiyo ianze, tayari wamekwisha wahudumia wagonjwa 27 na kwamba bado wanaendelea kutoaelimu kwa jamii ili wale waliokuwa wakipewa rufaa kwenda kutiiwa hospitali nje ya nchi watibiwe katika taasisi hiyo ya MOI.
“Na tunaendelea na taratibu za kutoa matibabu, kufanya uchunguzi, hivyo mtu akipata matatizo akifika MOI atakutana na Madaktari bingwa watamuangalia na baada ya hapo watampeleka kwenye uchunguzi kujua tatizo la mshipa wa damu limetokea sehemu gani ya ubongo au sehemu gani ya uti wa mgongo,”amesema Rehani.
“Lakini pia kuna wale ambao wanakuwa wamepata uvimbe kwenye ubongo na wanahitajika kwenda kufanyiwa upasuaji wa kufungua fuvu, kwa kutumia mashine hii ina uwezo wa kutumia mpira kwenye kitundu kidogo na kwenda kufunga ile mishipa ya damu ambayo inaenda kwenye ule uvimbe ili kupunguza uwezekano wa mgonjwa wakati wa kufanyiwa upasuaji asivuje damu kwa wingi.”
“Kwa hiyo tunapofunga mishipa ya damu inarahisisha upasuaji kwa njia ya usalama zaidi.”
Ameeleza kabla ya taaisi hiyo kuanzisha huduma hiyo, Januari mwaka huu gharama za uchunguzi na matibabu ambazo watu walikuwa wakizitumia kwenda nje ya nchi kutibiwa zilikwa kubwa zaidi.
“Ukienda nje ya nchi kutibiwa ugonjwa huu, gharama za uchunguzi pekee ni Sh.milioni 10 hadi 15 na matibabu yake ni zaidi ya Sh.milioni 20,”ameeleza Rehani.
Ameongeza kuwa kuhusu gharama za uchunguzi kwa taasisi hiyo ni kuanzia Sh.milioni 2.5 hadi 4.5 kwenye hatua ya uchunguzi na kwamba hatua ya tiba bado wanaaendelea na uchunguzi kwenye kitengo hiki ili wajue gharama ya mataibabu.
July 08, 2021
Home
Unlabelled
MOI yaleta unafuu kwa wagonjwa wa kiharusi
MOI yaleta unafuu kwa wagonjwa wa kiharusi
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment