July 09, 2021

TMDA kutenga maeneo ya kuvutia sigara

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa  Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo akizungumza na Waandishi wa Habari.

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Dawa  na Vifaa Tiba (TMDA), imesema kuwa inatengeneza miongozo ya kutenga maeneo rasmi ya uvutaji sigara, kuweka alama za kukataza kuvuta.

Akizungumza jana katika  banda  lao  la maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya  ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Vijana  na Biashara Endelevu'

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Adam Fimbo amesema wameanza kusimamia sheria ya udhibiti wa tumbaku ya mwaka 2003 ilikuwepo lakini hakuna mamlaka ambayo ilipewa na Wizara kwa lengo la kudhibiti tumabuku hiyo.

Amesema kuanzia Aprili mwaka huu  wameanza rasmi kudhibiti bidhaa za tumbaku ambazo zinavutwa na haziruhusiwi hapa nchini.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa bidhaa hizo ni kama vile ugoro, zinazowekwa chini ya ulimi, tumbaku, zile za kupaka kwenye ngozi na kuberi.

Amesema zinazoruhusiwa ni zile za kuvuta na ambazo zinaruhusiwa kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 18, walichini ya umri huo hawaruhusiwi.

"Kazi yetu kubwa ni kudhibiti bidhaa hizi kuanzia Aprili mwaka huu. Nafahamu kuwa maeneo mengi nchini hayajatengwa maeneo ya kuvutia sigara," amesema.mkurigenzi huyo.

Amesema kuwa kazi yao kubwa ni kudhibiti bidhaa hizo ambapo walianza  Aprili mwaka huu.

ELIMU

Amesema kwa sasa wanachokifanya ni kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi na kazi kubwa ni kuzuia wale ambao bado hawajaanza kuvuta sigara au tumbaku.

" Wale ambao tayari wameshaanza tutaona namna ambavyo tutawashawishi wasiendelee kuvuta," amesema.

Ameongeza kuwa watawapatia elimu juu ya madhara ya uvutaji kuwa madhara yake yanasababisha saratani kwenye mapafu, koo na magonjwa yasiyoyakuambukizwa.

" Tunatengeneza miongozo ya kutenga maeneo rasmi ya uvutaji sigara,kuweka alama ya kwamba hapa haparuhusiwi kuvuta sigara," amesema Fimbo.

Amerleza kuwa kazi yao kubwa kubwa ni kuwaelekeza wale wenye maeneo yanayohusisha mkusanyiko wa watu wengi watenge maeneo hayo na wasimamie suala hilo.

Ameongeza kuwa kile kile ambacho kina leta athari kubwa kwa binadamu kitaalamu yule anaye vuta moshi wa singara ni sawa na anaye vuta.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kazi yao ni kuona namna ya kuelimisha wavutaji na ambao hawavuti  kwamba mtu anayempulizia moshi wa sigara una muathiri sawa na anaye vuta.

Amesema elimu inahitajika kwani watu ni waoga mtu anapovuta sigara anamwangali hawezi kumwambia asogee mbali ili aendelee kuvuta sigara yake.

"Mfano wanaonunua dukani anaomba kiberiti na kuwashia hapo hapo na kuvuta pia bila kujali afya za wengine lakini na wale waliopo hawawezi kumwambia  na hii inatokana na uelewa mdogo wa madhara ya moshi wa sigara," amesema.

Ameongeza kuwa lengo la kutoa elimu ni kulinda afya za jamii na kwamba wanafahamu sigara ni zao la kiuchumi wakulima wa tumbaku wameruhusiwa kufanya Biashara yao, watengenezaji wanatengeneza kila siku na kusambaza.

Fimbo amesema  mataifa yote duniani hayajawahi kuzuia matumizi ya sigara, wao kama mamlaka Kazi yao ni kuelimisha jamii juu ya madhara  hayo.

Amesema tumbaku ina madhara ndio maana imeandikwa onyo  hiyo inamkumbusha mtumiaji.

Fimbo amesema tumbaku ina urahimu ndio maana inamfanya mtu ashindwe kuacha kwani akianza tu ile hali anayoipata ni kama vile dawa za kulevya anadindwa kuacha.

"Huwezi kumwambia mvutaji sigara, tumbaku acha kuanzia leo au kesho atakuwa anakushangaa," amesema mkurugenzi huyo.

Amesema utaratibu wa kuwafanya watu hao ni kuwapatia vitu vya kupunguza ili waache taratibu ili itoke kwenye miili yao.

No comments:

Post a Comment

Pages