July 06, 2021

VETA kuongeza ubunifu kuendana na kasi ya uchumi viwanda

 

Mbunifu wa vifaa vya kufundishia somo la Sayansi kwa vitendo, Wellington Lyimo, akitoa maelezo kwa Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, alipotembelea banda la VETA katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).

 

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema inafanya kazi kwa wakati na kwamba taaluma  yao inaendelea kukua kila siku kulingana na  Teknolojia iliyopo ili iuendana na kasi ya uchumi wa viwanda.

Akizungumza jana katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Julias Nyerere,Mwenyekiti wa bodi ya VETA Peter Matuki amesema Mamalka hiyo inafanya kazi na wenye viwanda kwa lengo la kuongezwa ujuzi kwa wanafunzi wao.

Amesema, kipindi hiki cha maonesho ya 45 wamejipanga kuonesha bunifu zao mbalimbali ikiwemo,maabara inayotembea ambayo itaondoa changamoto kubwa kwa shule ambazo hazina maabara.

"Tumejipanga kuongeza uchumi katika sekta ya viwanda hasa kwa vijana wanaonza vyuo na hata waliopo kazini tayari,"amesema Matiku

Ameongeza kuwa hata wafanyakazi waliopo kazini kwa muda mrefu wanatakiwa wafike VETA kwa ajili ya kupata mafunzo mbalimbali ili kuongeza tija katika kazi yake.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk.Pancras Bujulu amesema katika maonesho ya mwaka huu wamejipanga kuonesha bidhaa za mikakati ikiwemo,vifaa vya  kilimo,viwanda na ufugaji.

Mamlaka hiyo imejiimarisha zaidi katika utoaji wa elimu kwa kuongeza vyuo 33 katika mikoa mbalimbali nchini na kufanya kuwa na jumla ya vyuo 71.

"Tanzania ni moja  ya nchi inayoendelea katika mapinduzi ya viwanda  kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha vyuo vya Sayansi na Teknolojia ili wanafunzi wajue zaidi masuala ya ubunifu ambayo yanakwenda sambasamba na uchumi wa viwanda,"amesema Dk.Bujulu.

Dk.Bujulu ameeleza kuwa     bunifu zao zinaongeza ufanisi zaidi katika jitihada za uchumi wa viwanda.

No comments:

Post a Comment

Pages