Na Talib Ussi
Wadau na wanaharakati wa utetezi wa haki za Wanawake, Vijana na Watoto wamefanya utafiti mdogo wa kupitia Sera ya Jinsia na Ujumuishi (Gender and Social inclusions Policy) ya Tume Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya mwaka 2015 ili kuona kama demokrasia imezingatiwa katika mchakato wa Uchaguzi nchini.
Wadau
hao ni pamoja na Mtandao wa Jinsia Zanzibar (ZGC), Jumuiya ya Wanawake
wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Chama Cha Wanasheria Wanawake
Zanzibar (ZAFELA), Jumuia inayojihusisha na kupambana na Changamoto
zinazowakabili Vijana Zanzibar (ZAFAYCO), Jumuia ya Vijana Zanzibar
(ZYF) na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar
(TAMWA, ZNZ) ambapo wamefanyakazi ya kuipitia Sera hiyo na kuona
mapungufu mbali mbali ikiwemo kutotekelezeka tangu kuanzishwa kwake
Februari, 2015.
Kwa mfano
kifungu kidogo cha pili (2.5) kiimeeleza namna ya ushirikishwaji wa
makundi yote katika jamii, wakiwemo wanawake, Vijana na watu wenye
Ulemavu katika mchakato mzima wa uchaguzi ikiwemo ugawaji wa majimbo,
elimu ya mpiga kura na mambo yote yanayohusiana na uchaguzi. Lakini
utafiti huo umegundua makundi hayo hayakushirikishwa ipasavyo kama
ilivyoelezwa kwenye sera.
Pia
sera hiyo katika kifungu 3.1 (a) imeeleza katika kipindi cha miaka
mitano ZEC itatoa mapendekezao ya kuwanyanyua wanawake, vijana na watu
wenye ulemavu katika uteuzi wa makamishna wa ZEC.
Tunafahamu
kuwa mamlaka ya uteuzi wa makamishna sio ZEC kwa kuwa imeainishwa na
katiba ya nchi kwamba mwenyekiti na wajumbe wengine wawili watateuliwa
na rais, ambapo kati ya hao lazima mmoja awe jaji na wajumbe wengine
wane watatoka katika vyama vya siasa ili kuhakikisha kwamba ZEC
inasimamia vyema sera ya jinsia na ujumuishi ilisema kwamba mara kwa
mara itakua inapendekeza kufanya marekebisho ya katiba ili masuala ya
jinsia na ujumuishi yaingie katika katiba na kuifanya sera hii
itekelezeke.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) bi Salma Saadat
amesema Sera hiyo ni nzuri lakini inahitaji kupangiwa mpango kazi ili
iweze kutekelezeka kwani kipengele kidogo Na 4.1 (C) kinasema siku ya
kupiga kura ZEC itaandaa sehemu maalum ya uangalizi wa watoto /kucheza
ili kuwawezesha wanawake kushiriki uchaguzi vizuri. lakini ZEC
hawajawahi kuandaa eneo hilo katika chaguzi zote zilizopita.
Pia
amesema utafiti huo umebaini kuwa kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi
Zanzibar haina usawa wa kijinsia, kwani ina wajumbe wanawake wanne
kati ya 24 ambao ni sawa na asilimia 16 na haikuwahusisha makundi yote
bali wanasiasa tu ndio waliyoingizwa kwenye kamati hiyo kupitia vyama
vyao.
Vile vile uwepo wa kamati hiyo ni wa muda
mfupi, huundwa wakati wa uchaguzi na uhai wake humalizika mara tu baada
ya uchaguzi kwisha na pia kamati hiyo haijawekewa muongozo wa
kushuhulikia malalamiko ya ZEC huivunjwa kamati hiyo. Wala haina
muongozo wa kutatua vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu wakati wa uchaguzi.
“Kuna
wanawake walifanyiwa vitendo vya udhalilishaji wakati wa Uchaguzi
lakini hawajui waende wapi kupeleka kesi zao, kwasababu kamati haina
mwongozo wa kutatua kesi za mtu mmoja mmoja, kamati inapokea kesi za
vyama vya siasa tu kwa mfano kesi ya ACT kuhusu kiongozi wao kupinga
kuwapo kwa kura za mapema” “ambapo alituhumiwa kuvuruga amani” Alisema
Bi Salma.
Aidha Wadau wamependekeza Sera ya jinsia
na Ujumisho ya ZEC ipitiwe tena pamoja na kuipangia mpango kazi ili
iweze kutekelezeka, wamesema ni vizuri ikawepo kamati ya maadili ambayo
shirikishi itakayojumuisha mwenyekiti na mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi.
Mwanasheria, Afisa kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, wajumbe
kutoka vyama vya siasa na mjumbe mmoja kutoka jeshi la polisi. Hivyo
wadau wamependekeza kuwa ni vyema kukawa na kamati mbili moja ya maadili
ambayo pamoja na wajumbe waliyotajwa hapo juu wawemo pia na wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu kama wawakilishi kutoka asasi za kiraia.
Kamati
ya pili iitwe kamati ya dhamana/uhusiano ya vyama vya siasa( Political
Party Liason Committee), ambayo itajumuisha wanasiasa kwa asilimia
kubwa ili kuangalia,kujadili, kushauri na kupendekeza utendaji mzuri wa
usimamizi wa mchakato mzima wa uchaguzi na mwenendo wa vyama vya siasa.
Vile
vile katika mapendekezo wadau wameomba katiba ya Zanzibar ya mwaka
1984 ifanyiwe marekebisho ili wanawake waweze kuteuliwa kwenye nafasi ya
Makamishna wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kwasababu katiba iliyopo sasa
haimlazimishi rais wa Zanzibar kuzingatia usawa wa jinsia wakati wa
kuteua makamishna wa Tume hiyo ZEC ambapo kwa sasa ZEC ina kamishna moja
tu, mwanamke kati ya saba, sawa na asilimia 14.

No comments:
Post a Comment