July 06, 2021

Watanzania washauriwa kuamini bidhaa za DIT



 Meneja Masoko wa Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam  (DIT Co Ltd), Benjamin Kamtawa, akimuelezea. Mkuu wa taasisi hiyo Prof. Preksedia Ndomba ndani  taa za barabarani za kuongozea magari na wavuka kwa miguu amnazo zimebuniwa na kutengenezwa DIT.



Na Asha Mwakyonde Dar es Salaam



TAASISI ya Teknolojia  Dar es Salaam (DIT),inaomba ushirika no hasa kutoka kwa wajasiriamali na Watanzania kuamini bidhaa zinazozaliehwa na taasisi hiyo.

Hayo yamesema jana  na Mkuu wa taasisi ya DIT  Prof. Preksedia Ndomba ndani ya Banda  lao kwenye maonyesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere yenye kaulimbiu ya  ' Uchumi wa Viwanda Ajira kwa Vijana  na Biashara Endelevu'

Prof. huyo amesema bidhaaa zinazozalishwa DIT  ni kama zile zinazotoka nje ya nchi na kwamba zinashindana na zile za Wachina watu hawaamini kuwa zinafanana.

"Waje tuongee wakizipenda bidhaa zetu tuwe tunazalisha kwa wingi ili zitatue changamoto za ajira kwa vijana wabunifu. Nawaalika wajasiriamali, taasisi wajue kuwa hapa ndio nyimbani," amesema.

Ameongeza kuwa wanabidhaa za ngozi za viatu mabegi hizo zote zinasalishwa.

Mkuu huyo ameeleza kuwa Kuna fursa ya vijana kwenda kufanya kazi na DIT  wanasutio ya Ubunifu, Desing Stutio ili wakitoka hapo wakaanzishe biashara zao.

Ameongeza kuwa kuwa huo sio wakati wa kuzingatia vyeti ingawa vinahitajika kila mtu anaye muhudumia anataka kujua wewe ni nani.

" Shughuli zetu zote tunazozifanya zinatakiwa zitatue changamoto za jamii hii  ndio dhana yetu tutafanya hivi kwa kuhakikisha mafunzo yetu ni ya vitendo zaidi hata wakifanya utafiti mwisho wa siku kuwe na mazoa yanaoonekana," amesema.

Prof.Ndomba ameongeza kuwa kimsingi banda lao na shughuli wanazilozifanya zinatakiwa kutambulika kwa kuwa wameamua kutatua changamoto kwa jamii.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Viwanda Dkt. John Msumba amesema kila maonyesho wanaenda na bishaa mpya na kwa mwaka huu wamepeleka mashine ya kuchakata plasitiki na kutengeneza vipuli.

Amesema hiyo ni mojawapo ya bidhaa ya kupunguza, kutunza mazingira na ile ya  studio  ya ubunifu bidhaa ambayo  wanamtaka mwanafunzi au mtu akiwa na wazo lake anatoka na bidhaa.

Dkt. Msumba amesema design studio inasaidia mtu kulichakata wazo lake na kuliweka katika mfumo mzuri na kumsaidia kutengeneza bishaa yake.

" Akiingia na wazo atatoka na bidhaa pia tuna bidhaa za ngozi za viatu, mabegi hizo zote kampuni yetu ndio inayofanya kazi hii ni bishaa ambazo zinatengenezwa na wanafunzi  wanapotoka na ujuzi wengi wanaenda kufungua kampuni " amesema.

Akizungunzia kampuni tanzu  (DIT co otd), Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo  Regina Kumba ameeleza kuwa ipo chini ya taasisi ya DIT na kazi yake ni kubiasharisha bunifu zote zinazobuniwa ndani ya kampuni.

" Kazi ya pili  ya kampuni hii ni kutoa nafasi kwa vijana ambao wapo chuoni kupata maeneo ya kufanyia mafunzo kwa vitendo  tunatumia kampuni kuwapeleka sokoni na kwenye kazi ambazo tunazipata kama taasisi " amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages