Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imenyakua ushindi wa kwanza katika kundi Utafiti na Maendeleo katika Maonesho yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Dk. Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambako Mkutano Mkuu wa 18 wa Wahandisi nchini umefanyika.
Ushindi huo umepatikana baada ya watathmini kuridhishwa na viwango vya juu vya matokeo ya tafiti na bunifu zenye kutatua changamoto za jamii kuonyeshwa na wataalam kutoka DIT.
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano Mkuu wa DIT, Amani Kakana, Maonesho haya yametia wadau mbalimbali waliotembelea banda la DIT kutokana na tafiti na bunifu ambazo zimeletwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho baada ya kukamilika.
Naye Afisa Uhusiano wa Kampuni Tanzu ya Taasisi hiyo (DIT Co. LTD), Regina Kumba amesema kuwa kazi ya kampuni kuzibiasharisha bunifu hizo na kuhakikisha zinaingia sokoni kwenda kutatua changamoto katika jamii.
No comments:
Post a Comment