September 26, 2021

GEITA YATUA SALAMA LINDI

Wachezaji wa timu ya Geita Gold FC "WANANZENGO wa Kanda ya Ziwa " wakifanya mazoezi mepesi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo utakaochezwa Septemba 27, 2021.
Timu ya Soka ya Geita Gold FC "WANANZENGO wa Kanda ya Ziwa " imefika salama Lindi.

Timu hiyo iliyo chini ya kocha mzowefu Etienne Nndaryagije inatarajiwa kufanya mazoezi mepesi jioni hii kabla ya kufungua DIMBA na Namungo hapo kesho.

Akizungumzia mchezo huo Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, George Mbiligenda amesema timu ipo katika hali nzuri  na hakuna mchezaji wala mwalimu aliyepata tatizo la kiafya ama dhoruba ya safari.

"Tumefika salama Lindi na leo jioni tunataraji kufanya mazoezi mepesi kuzoweya uwanja tayari kuanza safari ya Ligi kuu 2021/2022" Alisema George.

Naye Mwalimu wa Kikosi hicho Etienne Nndaryagije amesema Anaiheshimu Namungo kutokana na kuwa uzowefu wakutosha katika Ligi lakini naye aanakikosi Cha vijana wenye uchu wa mafanikio na anategemea kupata ushindi

No comments:

Post a Comment

Pages