September 05, 2021

KAMPENI YA KUHAMASISHA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA UONGOZI YAANZISHWA ZANZIBAR

 Mkurugenzi wa Jumua ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud alipokia akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi huo.

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya uhamasishaji jamii kuwaunga mkono wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi wakifurahi baada ya kumaliza uzinduzi huo.


Na Talib Ussi  Zanzibar

 

Wanaharakati Visiwani Zanzibar wameazisha kampeni maalum ya kuwahamasisha wanawake kushiriki katika uongozi wa Serikali kwa kuandaa mkutano maalumu wa uzinduzi wa uhamasishaji huo.


Uzinduzi wa mkutano huo uliofanyika Viwanja vya Mnara wa kumbukumbu wa Mapinduzi ya Zanzibar Michenzani  Mjini Unguja ambapo Mkuu wa Wilaya ya Magharib A Unguja Suzan Petar Kunambi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi alisema anaamini kuwa  ifikapo mwaka 2030 Zanzibar tayari itakua na idadi kubwa ya viongozi wengi wanawake katika nafasi za juu Serikali.


Alisema kuongezeka Viongozi wanawake ni  kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na wanaharakati kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari wanawake kwa upande wa Zanzibar  TAMWA-ZNZ.

 
“Jamii isituchukulie powa sisi waanawake tunauwezo wa kuongoza sehemu yoyote ile iwe Serikalini au katika jamii, leo mnaona ndio tuliokamata kiti cha Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania” aliseema Suzan.
 
Alielezae hatua hiyo ya wanaharakaati kuandaa mkutano kuwa ni hatua muhimu ya kumkomboa mwanamke na jamii kuelewa kuwa mwanamke ni mtu muhimu katika taifa.

Alisema wanawake wamejaaliwa uwaminifu wa hali ya juu kuazia katika familia na hata jamii pamoja na nchi kwa ujumla.
 
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Wilaya alisema  kufanyika kwa mkutano huo wa uzinduzi ni kwenda sambamba na dira ya Serikali katika kuwajengea uwezo wanawake walio wengi kusimama kama viongozi kwenye Serikali au hata nje ya serikali.

Awali Mkururugenzi wa Jumuia ya Wanasheria wanawake Zanzibar (ZAFELA)Jamila Mahmoud alisema uzinduzi huo umekuja baada ya kupatikana kwa vijana 60 ambao waliwafanyia mafunzo maalumu ya kuwajenga wanawake kiuongozi ambao nao watakwenda kutoa mafunzo hayo katika maeneo yote ya Unguja.
 
Alisema vijana hao watafanya kazi kwa kila shehia za Mikoa yote ya Unguja huku lengo kuu likiwa ni kujengea uwelewa jamii juu ya ushirikishwaji wa wanawake kwenye nafasi za uongozi ziwe za kiserikali au hata za kijamii.
 
Awali akizungumza kwa niaba ya vijana ambao wamehitimu mafunzo hayo Fransisca Claimant alisema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa na wapo tayari kuyafanyia kazi na hatimae elimu hio kuifikia jamii.

Mradi  wa uhamasishaji wanawake kushiriki nafasi za uongozi ni wa miaka mine na unatekelezwa na TAMWA-ZNZ,kwa kushirikiana na ZAFELA pamoja na PEGAO chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages