September 27, 2021

KUMEKUCHA TPL, MOTO KWA MOTO MIAMBA 16 KAZI IENDELEE

 

Kikosi cha Azam FC kikifanya mazoezi mepesi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga utakaofanyika Septemba 28 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini humo.

 

Na John Marwa

Ukisikia paah ujue imekukosa, ukisikia pyeee ujue kumekucha, viwanja vinamelemeta, nyasi zinashangweka kuzipokea klabu 16 katika mbio mpya za kumsaka bingwa wa TPL 2021/2020.

Ni Ligi Kuu Soka Tanzania Bara TPL msimu wa 2021/2022 kuanza leo kwa mechi tatu kulindima, dakika 270 kuubariki msimu mpya.

Swali ni je nani kuibuka na pointi 90 ama kuongoza kwa pointi nyingi juu ya wenzake baada ya michezo 30 ya nyumbani na ugenini?

Nani kuacha mamilioni ya Azam Tv na kurejea Championship? Kazi kazi, mtoto hatumwi dukani ni michalazo tu!

Dakika 270 za Michezo mitatu Leo itatoa picha na matarajio ya wengi katika msimu huu??? Ni jambo linalosubiriwa kutimia ama kufikiwa baada ya michezo 240?!

Swali ni je nani kuibuka kinara wa mabao baada ya dakika 21,600? Nani kuibuka mtoa assist nyingi baada ya sekunde milioni 1,296,000? Nani kuibuka mchezaji bora, nani kuibuka na clean sheet nyingi?

Basi majibu yote yanaanza kujibiwa leo, ambapo Mtibwa Sugar watawaalika wageni wa Ligi Mbeya Kwanza, Namungo FC wauaji wa Kusini wakiwaalika wachimba madini wa Geita Gold FC na Wagosi wa Kaya wakiziwida ice cream za Azam FC.

Karibu sana TPL, karibu burudani ya Soka la Tanzania lenye maisha yake ya Dunia yake, karibu Ligi ya malalamiko, karibu TPL inayomkosa mchezaji bora kwa msimu miwili mtawalia Clatous Chota Chama na Luis Josee Miquissone Chuma cha Kimakonde.

Karibu sana TPL yenye Khalid Aucho, Yanick Bangala, Peter Banda, Ousmane Sakho, Dancan Nyoni, Saido Konoute na Shaban Djuma.

Karibu sana TPL itakayo shuhudia mechi za usiku nje ya Jiji la Dar es Salaam.

Furaha inaweza kupatikana kwa haki na maumivu yakapatikana kwa haki ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake.

Karibu TPL 2021/2020

No comments:

Post a Comment

Pages