September 21, 2021

NMB yakabidhi zawadi kwa mshindi wa CDF Trophy

 

  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Mathew Edwardo Mkingule akimkabidhi kikombe na zawadi Mshindi wa jumla wa mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi 2021, Victor Joseph yaliyofanyika kwenye viwanja vya TPDF Golf Lugalo na kudhaminiwa na Benki ya NMB. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara na Serikali, Alfred Shayo na wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Golf Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo.


Benki ya NMB imesema kuwa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) linastahili pongezi  kwa jinsi linavyozidi kuutangaza mchezo  wa gofu hapa nchini.

 

Hayo yalisemwa juzi usiku na Afisa mkuu wa wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shayo,  kwenye tafrija ya utoaji zawadi kwa washindi wa mashindano ya NMB CDF trophy  yaliyofanyika  kwenye viwanja vya  gofu vya  Lugalo.

 

Alisema mashindano  ya kombe ya mkuu wa majeshi ni moja kati ya mashindano makubwa ya gofu nchini, yamevutia wengi wanajeshi na  raia na kufanya wachezaji waweze kuongezeka.  

 

“Michezo sasa ni ajira yenye kulipa sana duniani, hivyo kwa kuzalisha wacheza gofu wengi zaidi, tunasaidia kuzalisha ajira kwa watanzania wenzetu.

“Kwa miaka sita sasa, tumekuwa pamoja na nikuhakikishieni tu , benki ya NMB bado ipo pamoja nanyi katika mashindano haya na tutazidi kuboresha udhamini wetu kwa kadri mahitaji yatakapo ongezeka.” alisema Shayo.

 

Akizungumizia udhamini wa benki ya NMB, imeweza kugharimia vifaa na  fedha taslimu kwa ajili ya kununua zawadi vyenye  thamani ya shilingi milioni 60.

 

Kwa mjibu wa Shayo akisema benki ya NMB imekuwa mdau wa michezo ya aina mbalimbali  nchini, “ kwa mchezo wa gofu  tumekuwa washirika wa muda mrefu ya kilabu ya Gofu ya Lugalo na wadau wakubwa wa mashindano haya ya mkuu wa majeshi,” alisema Shayo.

 

Mashindano hayo ya gofu ya mkuu wa majeshi nchini yajulikanayo “NMB CDF trophy” yalishirikisha wachezaji zaidi ya 150 kutoka vilabu vyote vya Tanzania.

 

Katika mashindano hayo  naodha wa timu ya taifa ya Tanzania Victor Joseph alibuka na ushindi wa mashindano hayo baada ya kupata grosi 141 akifuatiwa na Aldo Gandye aliyepata grosi 154.

 

Kwa upande wa upigaji wa mipira ya neti, Amri Kangajaka aliweza kushinda ushindi wa Jumla baada ya kupiga mikwaju ya neti 141 akifuatiwa na Elisha fadhiri aliyepata neti 143.

 

Upande wa Divison A  Petar Fiwa aliweza kushinda baada ya kupiga mikwaju ya neti 150 akifuatiwa na Damasi Gaitana aliyepata neti 152.

 

Kwa upande wa Division B  Lunacho Lugome aliibuka na ushindi baada ya kupiga mikwaju ya neti 145, akifuatiwa na Hussein Dewji aliyepata neti 145.

Upande  Dision C Vitalis Magere aliweza kushinda baada ya kupiga mikwaju neti 149 akifuatiwa na Dotto Bahenge aliyepata neti 152.

 na upande wa wanawake nafasi hiyo ilichukuliwa  Zuhura Shemdolwa  aliyepata neti 143.

 

Kwa upande wa upiganji wa mipira ya Longest Drive upande wa wanaume ilichukuliwa Isiack Daudi na wanawake ilichukuliwa Hawa Wanyeche..

Upande wa upigaji wa mpira uliokwenda karibu na shimo  upande wanaume ilichukuliwa Teddy Kalinga,

Kwa upande wachezaji wa kulipwa nafasi ya kwanza ilichuliwa na Frank Mwinuka  aliyepata grosi 140,  huku Abdalah Yusuph akiwa wa pili baada ya kupata grosi  150.  

No comments:

Post a Comment

Pages