September 09, 2021

ROSE MUHANDO KUWASHA MOTO TAMASHA LA KUMSHUKURU MUNGU

 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 9, 2021 wakati akitambulisha waimbaji wa nyimbo za injili watakaopanda jukwaani katika Tamasha la Kumshukuru Mungu litakalofanyika Oktoba 31, 2021. Kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, Emmanuel Mabisa. (Picha na John Dande).

 

Na John Dande, Dar es Salaam

 

Maandalizi ya Tamasha la Kumshukuru Mungu yamezidi kupamba moto huku waandaaji wakibainisha uwepo wa mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Rose Muhando. 

 

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo leo Agosti 9, 2021, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, amesema Rose Muhando ataungana na nyota wengine kama Martha Baraka pamoja na Martha Mwaipaja ambao wote wamethibitisha leo kushiriki katika tamasha la kihistoria la kumshukuru Mungu.

 

Waimbaji wengine mpaka sasa waliothibisha kushiriki katika tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 31 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ni Boniface Mwaitege, Christopher Mwahangila, Upendo Nkone, Jessica Honore, Messi Chengula pamoja na Enock Jonas.

No comments:

Post a Comment

Pages