September 14, 2021

Serikali kukabiliana na changamoto ya upotevu wa mazao





 

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


Serikali kwa ushirikiano na  wadau wake wa maendeleo katika Sekta ya uvuvi inakusudia kupambana na mojawapo ya changamoto za upotevu wa mazao yanayotokana na uvuvi ambayo yanafikia asilimia arobaini kabla ya kufika kwa mlaji.

Akizungumza  kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na uvuvi , Mkurugenzi wa ukuzaji viumbe maji, Dkt Nazael Madalla amewaambia wadau wa sekta ya uvuzi katika Ziwa Tanganyika kuwa mradi wa FISH4ACP  unaotekelezwa katika nchi 12 za Africa, Caribbean na Pacific unalenga kukabili changamoto  za upotevu wa mazao ya samaki kabla na baada ya shughuli za uvuvi, wakati wa uchakataji wa samaki na wakati wa kusafirishwa kwenda kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
 
Katika mkutano wa wadau wa uvuvi uliolenga kujadili na kuthibitisha matokeo ya utafiti wa mnyororo wa thamani wa dagaa na migebuka katika Ziwa Tanganyika na kubainisha changamoto wanazokabiliana nazo, Dk Madalla amesema  hatua hiyo itasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo katika shughuli za uvuvi kuanzia hatua za mwanzo kutoka kwa mvuvi hadi samaki wanapofikishwa mezani kwa hatua ya mwisho ya mlaji.
 
Amesema miongoni mwa hatua zinazotarajiwa kuboreshwa katika mnyororo wa thamani, ni pamoja  na kuangalia uwezekano wa kunzisha viwanda vya uchakataji, kuinua hali ya maisha ya mvuvi  kwa njia ya mikopo nafuu ili kuboresha zana za uvuvi, kuboresha miundombinu ya usafirishaji samaki, kujenga ushindani wa kibiashara kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa aina zote.  

Dk Madalla amesema dagaa ndio mazao yanayopotea zaidi kwa asilimia 40 hasa kipindi cha mvua kutokana na kutegemea jua katika ukaukaji wake ili ziweze kwenda sokoni.
 
Katika mchango wao,Wadau sekta ya uvuvi walipata fursa ya  kupitia taarifa za awali za matokeo ya utafiti, kujadili na kuthibitisha matokeo ya utafiti huo unaolenga kufahamu kwa undani fursa, changamoto na hatua za msingi za kuanza utekelezaji wa mradi huo mkubwa katika kipindi cha miaka minne kuanzia  mwakani.
 
Wadau wa Uvuvi wameiomba serikali  pamoja na wadau wake wa maendeleo kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ambao itasaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili.
 
" Tunachangamoto mbalimbali zinazotukabili kama wavuvi na wafanyabiasha, masoko ni tatizo lakini pia hatuna mialo ya kuanikia mazao yetu kama dagaa ndio maana hatuwezi kupata bidhaa bora ukilinganisha na maeneo mengine,"amesema Francis John.
 
Mfanyabiashara wa mazao ya uvuvi katika mwalo wa Kibirizi, Kigoma Said Idd Alli lito shukrani kwa Serikali kuja na mradi wa ukombozi kwa wavuvi wa hali ya chini unaolenga kuinua hali ya kipato cha mvumi kwa kutuwezesh kupata masoko ya mazao ya uvuvi ndani na nje ya nchi,  kuboresha zana za uvuvi na hivyo kutuvusha hatua moja kwenda nyingine, “Mvuvi katika Ziwa Tanganyika anavua hadi anazeeka akiwa na hali duni ya maisha kutokana na kazi ya hasara misimu yote ya mvua,”

Suzana Ezekiel ni mvuvi katika mwalo wa Kibirizi anaunga mkono hatua za ushirikishwaji wavuvi wadogo huku akiamini hatua hiyo italeta ukombozi kwa wavuvi wadogo. “Hakuna mvumvi wa Ziwa Tanganyika mwenye maisha mazuri hata ukiwa na mtaji mkubwa. Kila mara changamoto zinakwamisha maendeleo ya kazi za uvuvi. Jambo hilo linasababisha wazazi kushindwa kulipia hata ada za shule kwa watoto wetu.”

Kwa upande wake Mtaalam wa uvuvi kutoka FAO, Hashim Muumin amesema mojawapo ya malengo ya mradi huo ni kuimarisha lishe kwa wananchi wa wanaozunguka ziwa Tanganyika ili kuondokana na tatizo la utapiamlo katika jamii. amesema wanaenda kufanyia kazi maoni ya wadau walioyakusanya lengo kuwaongeza thamani katika sekta ya uvuvi.

Muumini amesema ulaji wa Samaki kwa mtu mmoja mmoja ni Mdogo lakini kuna kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu na walaji wanapendelea zaidi migebuka kuliko aina nyingine za Samaki tofauti na kuhe pia bei ya migebuka ni rahisi.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Dk Ismael Kimerei amesema mtu akitumia mazao hayo kwa sasa hawezi kupata virutubisho vya kutosha vilivyokisudiwa mwilini kutokana na kuandaliwa chini ya kiwango.
 
Mapema Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya TAFIRI, aliwaambia washiriki wa warsha hiyo kuwa wanalo jukumu la kujadili na kuthibitisha utafiti uliofanywa kufuatilia mnyororo wa thamani kwa uvuvi wa mazao ya samaki aina ya migebuka na dagaa katika Ziwa Tanganyika. 

Dk Kimerei  alisema utafiti huo umebainisha aina ya uvuvi unaofanyika Ziwa Tanganyika kuwa ni uvuvi mdogo mdogo unoendeshwa na wavuvi wenye zana duni na kwamba uvuvi huo bado haujahodhiwa na wavuvi wakubwa.
 
Alisema mradi wa FISH4ACP unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano na kwamba mwaka wa kwanza (2020/2021) mradi umeshughulika na utafiti kubainisha wadau wa sekta hiyo, shughuli zao, changamoto zinazowakabili, maoni yao ili kuelewa aina ya uwekezaji,  ramani walipo, mahala pa kuanzia ili kuhkikish shughuli za uvuvi katika  ziwa Tanganyika  zinakuja  endelevu, “Tutakuja na mpango kazi wa miaka minne tukilenga kujikita katika utekelezji wa mradi kikamilifu.” Dk Kimerei alifafanua.

Aidha amesema  waliweza kuwafikia watu 500 katika utafiti wao na kwamba katika utafiti huo waliweza kubaini biashara ya mazao ya uvuvi inafanywa na watu wa hali ya chini hivyo.
 
Amesema utafiti huo utasaidia kuwapa matokeo chanya yatakayowasaidia kuwaboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiasha na wavuvi katika ziwa Tanganyika.
 

No comments:

Post a Comment

Pages