September 14, 2021

Serikali ya Marekani imesambaza vyandarua vyenye dawa 630,000 kuwalinda vyema Wazanzibari milioni 1.3 dhidi ya malaria


Wiki iliyopita, serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ilikamilisha usambazaji wa takriban vyandarua vyenye dawa 630,000 na kufikia kila
kaya iliyosajiliwa kupata vyandarua hivi visiwani Zanzibar. 

 

Vyandarua vilinunuliwa kupitia Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Malaria (PMI), na Mfuko wa Kupambana na
UKIMWI pamoja na Kifua Kikuu na Malaria Duniani ambalo shirika la kimataifa la ufadhili na ushirikiano. 

 

Inatarajiwa kwamba kila chandarua chenye dawa kitawalinda watu wawili dhidi ya
malaria.


Malaria husababishwa na vimelea vya seli moja ambayo huingia kwenye damu ya mtu kufuatia kuumwa na mbu wa kike wa Anofelesi mwenye maambukizi. 

 

Katika miaka ya hivi karibuni, Zanzibar imeonekana kuongezeka katika visa vilivyoripotiwa. Kati ya 2019 na 2020, idadi ya visa vya malaria vilivyosajiliwa iliongezeka kwa asilimia 68, ikionesha mlipuko ambao ulisababisha kuongezeka kwa usambazaji wa vyandarua.


Vyandarua vyenye dawa vimethibitishwa kupunguza ugonjwa wa malaria, ugonjwa mkali, na vifo kutokana na malaria kwa kulinda watu dhidi ya kuumwa na mbu wakati wa kulala.


Vyandarua vyenye dawa vinadumisha viwango bora vya dawa ya kuua mbu kwa takriban miaka mitatu, hata baada ya kufua mara kwa mara. Maendeleo makubwa ya Tanzania dhidi ya malaria
yameainishwa katika Ripoti ya miaka 15 ya PMI. Kwa mfano, umiliki wa vyandarua vyenye dawa umeongezeka hadi asilimia 78 (kutoka asilimia 23 mwaka 2005).


PMI imekuwa mshirika maarufu wa Tanzania tangu 2006, kusaidia kupunguza viwango vya vifo vya watoto kwa asilimia 40 kupitia uwekezaji wa jumla ya takribani Dola za Marekani milioni 613 kufikia mwaka jana. Katika miaka minne tu iliyopita, dola milioni 176 zimetolewa kutoa dawa za kuokoa maisha, upimaji wa hali ya juu wa uchunguzi wa malaria na utoaji mafunzo kwa wafanyakazi wa afya zaidi ya 4,700.

 

 Kupitia ushirikiano wa karibu na watu, taasisi, na serikali za Tanzania na Zanzibar, serikali ya Marekani pia inaimarisha mifumo ya afya ili kuimarisha na kuongeza juhudi za Tanzania kumaliza ugonjwa huu hatari, lakini unaoweza kuzuilika kabisa.


Akitoa maoni juu ya mafanikio yaliyotokana na kampeni ya usambazaji wa vyandarua vyenye dawa, Mkurugenzi Mkazi wa USAID V. Kate Somvongsiri alisema " Serikali za Tanzania na Zanzibar zimepiga hatua kubwa na ya kutia moyo katika kuboresha ubora na utoaji wa huduma za malaria katika miaka kadhaa iliyopita. Ushirikiano wetu wa karibu unapunguza vifo vya malaria na kupunguza kwa kiwango kikubwa kuenea kwa malaria, lengo la muda mrefu likiwa ni
kuitokomeza kabisa.”

No comments:

Post a Comment

Pages