Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, akiwasha umeme katika nyumba ya Bi Georgia Joseph.
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Wananchi katika mtaa wa Kagondo kaluguru manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kuunganishiwa umeme baada ya kuishi muda mrefu bila huduma hiyo.
Akiwasha umeme katika makazi ya wananchi wa mtaa wa Kagondo kaluguru naibu waziri wa nishati na mbunge wa jimbo la Bukoba Stephen Byabato amesema mchakato unaoendelea kwa wizara hiyo ni kuangalia namna bora ya kuondoa gharama za juu za umeme kwa njia ya LUKU kwa wateja wapya.
Miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo waliofanikiwa kuunganishiwa huduma hiyo ni pamoja na Bi Georgia Joseph ambaye amesema kwa muda mrefu amekosa huduma hiyo jambo liliwafanya watoto wake kusomea katika mwanga wa vibatari wakiwa nyumbani.
"Namshukuru Mungu naishukuru serikali kupitia naibu waziri wa nishati kwa kutatua changamoto hii najua ameisemea sana huko bungeni naahidi tutatumia umeme kwa manufaa zaidi" alisema Bi Georgia.
Byabato amesema kuwa ameamua kuanza na baadhi ya maeneo katika Manispaa hiyo lakini akimini kuwa maeneo mengi bado yanahitaji umeme na kuwa anatambua TANESCO hawalali hivyo juhudi kubwa zinazofanyika katika kufikia malengo.
"Haikuniingia akilini kuona mji wa Bukoba unaendelea kukosa huduma hii nitahakikisha kila maeneo huduma hiyo inafika labda mwananchi ashindwe mwenyewe kuunganisha huduma hiyo wakati ambao tunaendelea na majadiliano na TANESCO juu ya Tarrif kwa wateja wapya" alisema Byabato.
Hata hivyo pamoja na uzinduzi wa tukio hilo amesisitiza kiwango sahihi cha shilingi elfu 27 kuendelea kutumika kwa kila anayehitaji huduma hiyo huku akisisitiza wananchi kuweka miundombinu katika nyumba zao ili wawashiwe umeme.
No comments:
Post a Comment