Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa akitoa agizo kwa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuandaa mpango mkakati wa makusanyo ya mirabaha kwa mwaka 2021/2022 na takwimu za maeneo yanayotakiwa kulipa mirabaha leo Septemba 10, 2021 katika kikao chake na kikosi kazi cha Kilichokuwa kikikusanya maoni ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma 2021 kutoka COSOTA leo Septemba 10,2021 Jijini Dodoma.
Na Anitha Jonas, Dodoma
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ameigiza
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuandaa mpango mkakati wa
makusanyo ya mirabaha pamoja na takwimu za maeneo yanayotakiwa kulipa
mirabaha na kuziwasilisha wizarani mwisho mwa mwezi Septemba.
Waziri
Bashungwa ametoa agizo hilo leo Septemba 10, 2021 Jijini Dodoma katika
kikao chake na Kikosi kazi cha kukusanya maoni ya wadau katika Kanuni ya
Leseni na Maonesho kwa Umma ya 2021 kutoka COSOTA kikiwasilisha taarifa
ya maoni ya wadau kwa kanuni hiyo.
"Katika kikao ambacho
tutakutana baada ya wiki mbili hizi mje na mkakati huo lazima tujue
tunakusanya kwa akina nani na wako wapi pamoja na idadi yao, pia
ongezeni kasi ya ukusanyaji wa mirabaha Disemba tunatakiwa kutoa gawio
kubwa,"alisema Mhe. Bashungwa.
Amesisitiza kuwa anahitaji
kupata makadirio ya makusanyo ya mirabaha hiyo kwa mwaka huu wa fedha
na kuanzisha utaratibu ambao atakuwa akifuatilia hali ya makusanyo
hayo kwa kila mwezi kwa kuhakikisha anapata taarifa.
Pamoja
na hayo naye Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Pauline Gekul aliitaka COSOTA kuhakikisha inajipanga zaidi na kujenga
utaratibu wa kushirikiana na mashirikisho na vyama vinavyosimamia maeneo
ya kukusanya mirabaha ili kutengeneza mazingira rafiki ya zoezi hili la
ukusanyaji.
Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi alifafanua kuhusu suala la
kukamilika kwa mfumo utakao kuwa ukihesabu na kutambua nyimbo
zinazochezwa katika vituo vya Redio kuwa unatarajia kukamilika mwezi
Oktoba na ndiyo utaanza kufanya kazi rasmi.
" COSOTA mna
kazi kubwa ya kufanya na kuhakikisha mnakusanya fedha za kutosha ili
gawio la mwezi Disemba liwe lenye hamasa kwa Wasanii wetu ni imani yangu
kuwa kwa Kanuni hii mpya na viwango hivi mlivyopanga kuwa vinalipika
kikubwa katika hili ni kuweka mifumo ya kiteknolojia ambayo itarahisisha
makusanyo hayo,"alisema Dkt.Abbasi.
No comments:
Post a Comment