October 05, 2021

Bihimba : watoto yatima wasikate tamaa ya kuishi jamii inawajali

 


Mkurugenzi wa Taasisi ya Bihimba Foundation Bihimba Mpaya (kulia), mwenye shati la bluu bahari akiwe katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Msongola Orphanece Trust Fund.


NA ASHA MWAKYONDE, DAR ES SALAAM
 

MKURUGENZI wa Taasisi ya Bihimba Foundation ,Bihimba Mpaya  anesema kuwa watoto yatima wanaolelewa katika vituo vya Kulelea watoto  hao wanahitaji faraja  ili wajione hawajatenga na jamii.

Akizungumzia jijini Dar es Salaam juzi wakati akitoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwamo vifaa vya shule katika kitu cha Kulelea watoto yatima cha Msongola  Orphanace Trust Fund kilichopo Kata ya Msongola Wilayani Temeke Bihimba amesema watoto hao wakitembelewa mara kwa mara wanajihisi wapo na wazazi wao.

Amesema kuwa kupitia taasisi hiyo kwa kushirikiana na tMaandao wa 24 technical Radio& kujoka tv wametoa msaada huo  ili kuwawezesha watoto  hao  48 wanaolelewa katika kituo hicho nao wajisikie kuwa  hawajatenga na jamii yao.

"Nimeweza tena kukabidhi, vyakula mbalimbali na vifaa vya shule ili viweze kuwasaidia watoto hawa  kwani hata mimi Sina baba wala mama wazazi  wangu walifariki nikiwa darasa la tatu shule ya msingi kichangachui iliyopo Kigoma Ujiji  nikiwa  darasa la tatu,"anesema Bihimba.

Bihimba amevitaja vitu hivyo kuwa ni vifaa vya shule, sukari, nyama, Maharage, sabuni ,mikate na unga wa sembe.

Mkurugenzi huyo ameongeza kupitia Bihimba Foundation atakuwa anawatembelea  watoto hao mara kwa mara na kuwasaidia misaada mbalimbali wanao hitaji.

Aidha Bihimba amewashauri watoto hao kwamba  wasivunjike mioyo  kwa kuishi yatima na badala yake wasome kwa bidii.


 

No comments:

Post a Comment

Pages