October 07, 2021

CAMP YA WANANCHI ARUSHA YAOTA MBAWA

Na Mwandishi Wetu

KWA mujibu wa Afisa habari wa klabu ya Young Africans, Hassan Bumbuli amesema, wamepewa ushauri na benchi la ufundi wameamua kuibakiza timu Dar es Salaam.

Wataendelea na program zote Avic Town, amesema benchi la ufundi limewashauri kubaki Dar es Salaam ili kuepusha usumbufu kwa Wachezaji watakaoanza kurejea kutoka kwenye timu zao za taifa.

Pia klabu hiyo imesema baada ya kutoka Songea kwenye mchezo dhidi ya KMC hawatarejea Dar es Salaam, mchezo wao dhidi ya Azam fc wataupeleka katika dimba la Shekh Amri Abeid Arusha.

No comments:

Post a Comment

Pages