October 13, 2021

CCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepongeza Mwenyekiti wa Chama hicho Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mapambano dhidi ya UVIKO19 huku kikitoa wito kwa Viongozi wa Kamati za Siasa kuanzia ngazi ya Shina hadi Mkoa kuhakikisha wana simamia kwa karibu mradi huo wa kupambana na UVIKO19 ili Fedha zilizotolewa zikatumike kwa malengo yaliyo kusudiwa.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Katibu wa NEC wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM,Shaka Hamdu Shaka wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema kuwa fedha zinazoenda kutekeleza Mradi  huo sio sadaka bali ni mkopo hivyo ni vyema wakatimiza majukumu yao ipasavyo.

Aidha amesema kwa watakokiuka matumizi ya Fedha hizo Chama kiatachuliliwa hatua Kali za Kisheria kwa Mujibu wa kanuni,taratibu na kanuni za Chama hicho.

Katika hatua nyingine,Katibu huyo amewapongeza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi  CCM katika Jimbo la Ushetu baada ya kulipa ushindi kwa kumchagua Peter Cherehani kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ambapo pia amekpongeza Chama  Cha ACT Wazalendo kushindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Konde Zanzibar.

Hata hivyo  amewataka viongozi  wa Kamati za siasa za chama hizo kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa kusimamima matumuzi  ya fedha hizo kikamilifu na ziende kutumika kama ilivyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Pages