October 13, 2021

Kampeni Temeke Gulio kuondoa Machinga barabarani

 


Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wafanyabiashara (Wamachinga) 


Na Mwandishi Wetu


WILAYA ya Temeke jijini Dar es Salaam imekuja Kampeni ya Temeke Gulio ambayo itatumika kuondoa wamachinga katika maeneo yasiruhusiwa kufanya biashara.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo ambapo alisisituza kuwa ifikapo  Octoba 18,2021 hataki kuona wapachinga wakiwa maeneo yasiyoruhusiwa.


Amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeshaweka utaratibu mzuri kwa ajili ya wafanyabiashara waliopo hivyo October 18 kila mfanyabiashara awe ameshahamia kwenye eneo sahihi. 


Amesema Manispaa ya Temeke imejenga masoko  mengi chini ya Mradi wa Kuendeleza jiji la Dar Es Salaam (DMDP), ambayo yalikuwa hayafanyi vizuri  hivyo baadhi ya wafanyabiashara watakwenda kufanyabiashara zako huko.


"Kwanza nawapongeza sana ndugu viongozi wa Wamachinga Temeke tunashirikiana vizuri  sana hivyo basi tuna maeneo 20 ambayo yametengwa kwa ajili yenu na hapa lazima nimshukuru sana Mkurugenzi wa Manispaa,  Elihuruma Mabelya kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika hili. "alisema.


Alifafanua kuwa maeneo mengine ambayo yametengwa Buza Makangarawe, Mbagala, Zakhem na maeneo mengine ambapo tayari wao kama viongozi wameshatoa maelekezo na elimu juu mchakato huo. 


Pia aliongeza  kuwa katika kuhakikisha wanaboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiasha halmashauri inakwenda kuzindua kampeni ya temeke gulio ambapo lengo kubwa nikutaka kuwaonyesha fursa mbalimbali za biashara na kuzifikia taasisi mbalimbali. 


"Ndugu wafanyabiashara gulio hili linakwenda kutoa fursa kwenu wafanyabiashara na tunatarajia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla atazindua rasmi gulio hili hivyo tushirikiane kwa ajili ya maendeleo ya Temeke yetu"alisema.


Amesema hadi hivi sasa wamewatambua wafanyabishara 5875 na kati ya hayo 1600 wameomba nafasi  nakwamba nafasi zilizobaki ni 3000  hivyo wafanyabishara wandelee kuchangamkia nafasi kwani hawatavumiliawatu wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi. 


Wakati huohuo Mkuu huyo wa wilaya Jokate alimpongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuweza kuwapatia shilingi bilioni tano kwa ajili  ya kutekeleza miradi mbalimbali iliyopo ndani ya wilaya hiyo ikiwamo kutatua changamoto ya madawati na madarasa ambapo mwaka ujao wanafunzi wote wa kidato cha kwaza wataingia kwa awamu moja.


Pia alisema fedha zingine zitakwenda kujenga Kituo cha Afya Mbagala, Tuangoma na zingine zitakwenda kujenga majengo ya huduma za dharura na pia zitakwenda kujenga bweni la Shule ya Sekondari Kibasila na nyingine zitakwenda kwenye mapambano dhidi ya Uvid-19.


"Hapa nisemme tu tunamshukuru sana sana Rais Samia, kwa kweli hapa niseme hadi ifikapo 2025 atakuwa amefanya mambo makubwa ya maendeleo kwa ajili ya Watanzani. "alisema


Kwaupande wake Mkurugenzi wa Halmashauri, Mabelya alimwahakikishia mkuu wa wilaya hiyo kuwa atahakikisha fedha zote zilizotolewa na Rais Samia zitafanya kazi zilitotarajiwa na haitaliwa hata senti moja.


Pia alimshukuru mkuu huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ndani ya wilaya na wao wataendelea kushirikiana naye katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa temeke.


Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya hiyo, Daniel Sayi alisema mambo yote yanayofanyika ni utekelezaji wa Ilani ya chama hivyo wao kama viongozi kazi kubwa nikuangalia na kusimamia ahadi zilizohaidiwa na viongozi kama zinatekelezwa ipasavyo.

No comments:

Post a Comment

Pages