October 18, 2021

MAHAFALI YA SABA YA SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA YA SULLIVAN PROVOST YA KIBAHA YAFANA

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa, akizungumza wakati wa mahafali ya Saba ya Kidato cha Nne ya shule hiyo iliyopo  Kibaha kwa Mathias Pwani. Kushoto ni  Afisa Mradi wa Teachers Juction, Njama Salim, pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Elifas Tozo Bisanda   ambae ndio alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Elifas Tozo Bisanda  (wa pili kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Wavulana  Sullivan Provost  Francis Kiango, cheti cha pongezi kwa kuongoza katika masomo yote wakati wa hafla ya mahafali ya  saba ya shule hiyo, hafla ya mahafali hayo yamefanyika shuleni hapo  Kibaha kwa Mathias, mkoani Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule hiyo, Rachel Mwalukasa.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Elifas Tozo Bisanda  (wa tatu kushoto) aliyekuwa mgeni rasmi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sondari ya wavulana ya Sullivan Provost, Rahim Ally (kulia), wakati wa mahafali ya saba ya shule hiyo, hafla ya mahafali hayo yamefanyika shuleni hapo  Kibaha kwa Mathias, mkoani Pwani hivi karibuni. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule hiyo, Rachel Mwalukasa na  Afisa Mradi wa Teachers Juction, Njama Salim.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa akikabidhi zawadi ya kitabu kwa mmoja ya wahitimu wa kidato cha nne wakati wa hafla ya mahafali ya saba ya shule hiyo iliyopo kibaha kwa mathias mkoani pwani.

No comments:

Post a Comment

Pages