HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 13, 2021

MOI yatumia utaalamu mpya kutibu watoto wenye kibiyongo


Wataalamu wa kutoka nchi za Palestina na Italia wakishirikiana na wataalamu wa Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), kumnyoosha mtoto mwenye tatizo la kibiyongo (haonekani pichani) kwa kutumia utaalamu mpya bila kufanyiwa upasuaji wowote.


Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam


WATOTO chini ya umri wa miaka 10 wenye tatizo la Kibiyongo  ' Scoliosis' wanepatiwa huduma ya kunyooshwa bila kufanyiwa upasuaji wowote kwa kutumia utaalamu mpya.


Inakadiriwa Watanzania 200,000 wanamatatizo ya kibiyongo na idadi ya wanaornda hospitalini kupata matibabu ni ndogo.


Akizuzungumza jijijini Dar es Salaam jana katika Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Respicious Boniface amesema wapo kwenye  kambi  ya pili ya  upasuaji ambayo imeanza juzi kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchi za Palestina na IItalia.


Mkurugenzi huyo alisema mbali na kambi hiyo nyingine ilifanyika miaka miwili iliyopita  na kwamba mwaka jana hawakuweza kufanya kwa sababu ya changamoto ya Corona.


Ameogeza kuwa mbali na watoto hao kuna wengine watano ambao umri wao umeenda  wao wanafanyiwa upasuaji na kuwekewa vipandikizi malaamu.


" Watoto watano hawatafanyiwa upasuaji watanyooshwa kwa kutumia  mbinu mpya waliyofuncishwa wataalamu wetu ya kutumia 'P.O.P'  mbinu hii ni mpya haihitaji upasuaji gharama zake zitakuwa ni nafuu," amesema Boniface.


Mkurugenzi huyo amesema kama mgonjwa wa kibiyongo angeenda nje kutibiwa ingemgharimu Mil. 100  ambapo katika Taasisi ya MOI anatibiwa kwa gharama ya Mil.40 na kwa watoto waliochini ya miaka 10 wananyooshwa kwa 350,000 hadi 400,000.


Ameongeza kuwa kwa mgonjwa wa kibiyongo mmoja anawekeza vipandikizi 18 ambapo kimoja kina gharimu  400,000.


"Kama mnakumbuka tuliandaa MOI Marathon lengo lake ni kukusanya fedha kwa ajili ya kununua  vipandikizi kwa sababu ni gharama Watanzania wengi hawataweza . Nawashukuru wote waliochangia  na ndio zinatumika sasa" ameeleza.


Ameeeleza kuwa kila mwaka wataalamu wa nje wanakuja nchini kwenye kambii za mafunzo kuwafundisha  mbinu mpya   za upasuaji  kwa kuwa udaktari ni sayansi.


"Tunashirikiana na wenzetu wa nchi zilizoendelea wao wameendelea wanapata mabadiliko mapema zaidi ikitokea kuna mbonu mpya ya upasuaji kila mwaka wanakuja  wanawafunfisha wataalamu wetu, " amesema.


Amesema  wataalamu wao  pia wanaenda nje ya nchi takribani miaka 10  kupata utaalamu  na kwamba kwenye kambi hiyo wanatarajia kutibu wagonjwa 10  wakubwa na watoto.


Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wazazi kuwa makini kuwaangalia watoto wao mapema  na kama wakiwaona mtoto akikaa mabega hayaobekani wawapeleke katika taasisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages