October 05, 2021

NAIBU WAZIRI HUSSEIN BASHE ATEMBELEA VITUO VYA KUNUNULIA MAHINDI SUMBAWANGA NA LAELA MKOANI RUKWA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiongozana na Kaimu Meneja wa TFRA Sumbawanga na Mpanda Bw. Range Marwa , Mbunge wa Jimbo la Kwera Mhe. Deus Sangu anayeongea na simu  pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali katika ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mahindi kupitia NFRA wilayani Sumbawanga

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Bw. Na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Milton Lupa , Mbunge wa Jimbo la Kwera Mhe. Deus Sangu na viongozi mbalimbali wa serikali katika ukaguzi wa zoezi la ununuzi wa mahindi kupitia NFRA wilayani Sumbawanga

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha Ufipa Bw. Adabeth Mbuyani kuacha kukopa fedha taslimu kwa mabenki kwa ajili ya kununulia mbolea wakati alipokagua ununuzi wa mahindi katika kituo cha Sumbawanga mkoani Rukwa akiwa kwenye ziara ya kikazi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akitoa maagizo kwa Mwenyekiti wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha Ufipa Bw. Adabeth Mbuyani kuacha kukopa fedha taslimu kwa mabenki kwa ajili ya kununulia mbolea wakati alipokagua ununuzi wa mahindi katika kituo cha Sumbawanga mkoani Rukwa akiwa kwenye ziara ya kikazi.

 Wakulima akina mama wakichambua mahindi yao tayari kuyauza kwa NFRA ghala la mahindi TFC Sumbawanga alipokuwa katika ziaya ya kikazi kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi unaofanywa na serikali kupitia NFRA

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akitoa maelekezo kwa wakulima wanaochambua mahindi yao tayari kuyauza kwa NFRA ghala la mahindi TCF Sumbawanga alipokuwa katika ziaya ya kikazi kukagua zoezi la ununuzi wa mahindi unaofanywa na serikali kupitia NFRA

Baadhi ya vibarua wakipakia mahindi kwenye gari katika ghala la TFC Laela ambapo NFRA imeweka kituo cha kununulia mahindi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na wauzaji wa mahindi wakati alipokagua ununuaji wa mahindi katika kituo cha NFRA Laela.

Baadhi ya akina mama wakichambua mahindi katika kituo cha kununulia mahindi cha Laela mkoani Rukwa.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiangalia ubora wa mahindi wakati alipokagua kituo cha kununulia mahindi cha Sumbawanga.

Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika ghala la TFC kituo cha kununulia mahindi cha NFRA Sumbawanga mjini.

No comments:

Post a Comment

Pages