Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe
kuzindua rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake
katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia. Uzinduzi huo
umefanyika leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto Waziri
wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi, wa pili kushoto Mwakilishi mkazi
wa UN Women hapa nchini bibi. Hodan
Addou, kulia Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg na Mwenyekiti wa Chama
cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea ujumbe
maalum kutoka kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda uliowasilishwa na Mjumbe Maalum
ambae pia ni Waziri wa Sayansi na Teknolojia na Ubunifu nchini Uganda Dkt.
Monica Musenero Masanza, Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Oktoba, 2021.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 28 Oktoba
2021 ameshiriki katika mjadala kuhusu Kipindi cha mpito wa haki wa tabianchi ulioendeshwa
kwa njia ya mtandao na Taasisi ya Mabadiliko Ulimwenguni, Tony Blair Institute
for Global Change.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg mara baada ya kuzindua
rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji
wa maamuzi na utendaji haki kwa familia, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe
28 Oktoba, 2021.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi
wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini
Dkt. Hodan Addo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA)
Jaji Joaquine De Mello baada ya kuzindua rasmi Mwongozo wa Mashauri kwa Majaji na
Mahakimu Wanawake katika kutekeleza utoaji wa maamuzi na utendaji haki kwa familia
leo tarehe 28 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment