October 15, 2021

WANAFUNZI WA VETA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO KIWANDA CHA TRANSFOMA CHA AFRICAB

Meneja uzalishaji wa Transifoma Kampuni ya Africab, Mhandisi Mumoti Lusinde (wa pili kushoto) akiwaonesha wanafunzi Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kipawa namna ya usukaji wa Transifoma walipofanya ziara ya kimafunzo katika kiwanda hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Mhandisi wa vizibiti umeme (Insulator) kutoka kampuni ya Africab, Festo Kinanda akiwatoa maelekezo kwa wanafunzi Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kipawa namna ya vifaa hivyop vinanvyo tengenezwa wakati wa ziara ya kimafunzo katika kiwanda hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Mzimamizi wa uzalishaji wa Transfoma katika kampuni ya Africab, Maliki Makata akitoa maelezo ya namna Transfoma inavyofanya kazi kwa wanafunzi Chuo cha Ufundi Stadi VETA Kipawa namna ya vifaa hivyop vinanvyo tengenezwa wakati wa ziara ya kimafunzo katika kiwanda hicho kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu


WANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi cha Veta Kipawa wametembelea kiwanda cha kuzalisha Transfoma cha  Africab kilichopo Kiwalani Dar es Salaam kujifunza kwa vitendo utengenezaji wa Tranfoma na vifaa mbalimbali vya umeme vinavyotengenezwa kiwandani hapo.

Wakizungumza wakati wa ziara hiyo baadhi ya wanafunzi hao walisema  imekuwa furaha kubwa kwao kuona namna uzalaishaji wa transfoma  unavyofanyika na kusisitiza kuwa kwao kumewasaidia kuongeza maarifa  ya darasani na hata baadae watakapohitimu masomo yao.

Mmoja wa wanafunzi hao Zuberi Issa anayesomea kozi ya umeme wa viwandani alisema amejifunza mengi kupitia ziara hiyo akiamini kuwa atatumia  ziara ya  mafunzo hayo kama sehemu ya maendeleo ya kozi yake darasani.

Alisema akiwa darasani wamekuwa wakifundishwa namna mballimbali ya utengenezaji wa transfoma  hali iliyomfanya kuwa na hamu ya kuona kwa vitendo namna ambavyo transfoma hizo zinatengenezwa  na hivyo kujiona kiu yake na wanafunzi wenzake imetimia.

Naye mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa kozi ya umeme wa viwandani Martina Urassa alisema  kwake ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa hasa baada ya kujfunza kwa vitendo  transfoma na vifaa vingine vya umeme vinavyotengenezwa akiamini kutamuongezea  ujuzi azaidi wa darasani.

Mbali na kuushukuru uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwapa nafasi hiyo ya wao kwenda kujifunza pia alitoa rai kwa wanafunzi wa vyuo vingine kutumia fursa  ya mafunzo inayotolewa na chuo hicho ili kujiongezea maarifa kama ilivyofanyika kwao na wanafunzi wa vyuo vingine.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja Uzalishaji wa African Mumoti Lusinde alisema ziara  ya wanafunzi hao ni muendelezo wa utaratibu wa kampuni hiyo kutoa nafasi kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kwenda kujifunza kwa vitendo namna bidhaa za kampuni hiyo zikiwemo Transfoma zinavyotengenezwa.

Alisema hatua hiyo ni utaratibu wa mara kwa mara unaofanywa na kampuni hiyo kutoa nafasi za wanafunzi kwenda kujifunza mambo  mbalimbali ya kiufundi kupitia viwanda vyake huku akisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo kunawawezesha  vijana kuwa na uelewa wa kutosha.

“Tunatoa rai kwa viwanda vingine kuiga mfano huu kwa kuwa kunawasaidia vijana wetu kuwa na uelewa wa kutosha na hivyo kuzalisha wataalamu wenye weledi wa kutosha watakaokuja kulisaidia Taifa  siku za baadae” alisema Lusinde

No comments:

Post a Comment

Pages